Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili unavyoneemesha, kutafuna wachezaji

Usajiliiiiii Usajili unavyoneemesha, kutafuna wachezaji

Thu, 13 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Tunashuhudia maisha ya wanasoka yakianza kubadilika mara wanaposaini mikataba ya kuchezea timu kubwa za Ligi Kuu za nchi mbalimbali kama ya Tanzania Bara, ambako timu vigogo ni Azam, Simba na Yanga.

Mchezaji aliyekuwa na maisha ya kawaida huanza kuonekana ananunua gari dogo na baadaye kununua kiwanja na mwaka mwingine anaonekana anaanza kujenga. Miaka yake mitano humtosha kujijengea msingi wa maisha na ikifia wakati ameyumba, kitachomtatiza ni mtiririko wa fedha kupungua na sasa anapoangukia kwenye timu ndogo wakati kiwango chake kinaposhuka.

Kiini cha kubadilika kwa haraka kwa maisha yake ni mkataba anaosaini na klabu yake pamoja na bonasi anazopata wakati msimu ukiendelea pamoja na zile za mwishoni mwa msimu zinazotokana na mafanikio ya jumla ya timu.

Wakati huu, dunia nzima iko kwenye usajili ambao umeongozwa na mshambuliaji nyota duniani, Kylian Mbappe aliyesajiliwa na Real Madrid ya Hispania akitokea Paris Saint Germain ya Ufaransa. Nchini Tanzania tayari klabu zimeanza kusajili wachezaji kwa ajili ya kuziba maeneo dhaifu au kuimarisha vikosi.

Ipo migogoro inayoweza kukwamisha mchezaji kuondoka kutokana na mikataba na zipo kesi zitakazoibuka baada ya baadhi kupewa mkono wa kwa heri bila ya kutimiziwa malipo yao.

Hayo yote hutokana na mikataba ambayo husainiwa wakati mchezaji anaposajiliwa.

Fuatana na David Skilling katika Makala hii inayoweza kusaidia kufumbua macho wachezaji kabla ya kusaini mikataba ili kujihakikishia kipato kizuri na kutumia fursa zinazotokana na kiwango chake uwanjani.

Kuanzia wakati mchezaji chipukizi anaposaini mkataba wake wa kwanza wa kucheza soka la kulipwa, mabadiliko hya kifedha yanaanza kuonekana. Wachezaji hao ambao wanakaribia miaka 20 au wameshavuka wanaingia kwenye dunia ambayo kiwango chao uwanjani kinahusishwa moja kwa moja na ujira wa kifedha.

Mkataba wake na klabu pamoja na wa kutumia taswira yake ndio vitu vinavyojenga msingi wa kipato chake, pamoja na nyongeza ya bonasi, kutangaza chapa za bidhaa na hivyo kuwa na uwezo wa kupata fedha nyingi.

Mwanasoka ni mwajiriwa halisi na analipwa kwa kadiri anavyofanya kazi. Hata hivyo, katika miaka ya karibuni, wachezaji wamepata uwezo mzuri zaidi wa kuelewa thamani ya haki za zao binafsi (image rights) na hivyo wameanza kufungua kampuni kwa ajili ya kushughulikia mikataba inayohusu mambo hayo. Tabia hii imekuwa ya kawaida miongoni mwa wanasoka nyota duniani.

Pamoja na kwamba uamuzi huo unawaongezea mzigo wa kodi, unasaidia kutengeneza mfumo mzuri wa kushughulia vyanzo tofauti vya mapato ya mchezaji.

Katika makala hii, David Skilling anaonyesha jinsi wachezaji wanavyojipatia mapato kutokana na mikataba wanayosaini na klabu na gharama zake.

MKATABA WA AJIRA

*Mshahara: Katika mihimili wa mapato ya mchezaji, mshahara ndio kitu muhimu na hukubaliwa katika mkataba na klabu. Mshahara huu hutakiwa kulipwa kwa mwezi au wiki na ndio chanzo imara cha fedha na kinachotabirika.

*Bonasi ya kusaini mkataba: Wakati wanaposaini mikataba, wachezaji wanapokea donge la fedha kama bonasi ya kusaini nyaraka hiyo. Mara nyingi fedha hizo huwa nyingi, hasa kwa uhamisho wa wachezaji nyota. Imeripotiwa kuwa mkataba wa miaka mitano wa mshambuliaji mpya wa Real Madrid, Kylian Mbappe umem uwezesha kupata Pauni milioni 12.7 za Kiingereza (sawa na Sh 42.3 bilioni za Kitanzania) kama mshahara wa mwaka na Pauni milioni 150 za Kiingereza (sawa na Sh. Bilioni 499.7 za Kitanzania) kama bonasi ya kusaini mkataba. Fedha ya bonasi imekuwa kubwa kwa sababu amesajiliwa kama mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wake PSG ya Ufaransa.

*Bonasi inayotokana na kiwango: Klabu huweka motisha kwa wachezaji kwa kuwaahidi bonasi ambazo ni pamoja na:

1. Bonasi ya kucheza mechi: Malipo kwa kila mechi anayocheza

2. Goli na pasi ya goli: Tuzo kwa kufunga bao au kutoa pasi ya mwisho—Inasadikiwa kuwa Mohamed Sallah alilipwa bonasi ya Pauni milioni 2.5 na Liverpool baada ya msimu wa kwanza kutokana na kuvunja rekodi ya kufunga zaidi ya mabao 30.

3. Kutoruhusu kufungwa goli: Kwa mabeki na makipa, bonasi hii hulipwa kutokana na timu kutoruhusu bao. Inasadikiwa beki Virgil Van Djik alijikusanyia Pauni 250,000 za Kiingereza (sawa na Sh. Milioni 832.9 za Kitanzania) kwa mechi ambazo Liverpool haikuruhusu bao.

4.Bonasi za ushindi na sare: Malipo zaidi kwa ushindi au sare.

5. Bonasi ya mafanikio ya timu: Wachezaji hupokea malipo yanayotokana na mafanikio ya jumla ya timu, kama kutwaa ubingwa wan chi, kombe la nchi, kusonga mbele kufikia hatua za juu katika mashindano kama Ligi ya Mabingwa. Kwa mwaka 2022/23, kila mchezaji wa Manchester City aliweka mfukoni Pauni milioni 2 za Kiingereza (sawa na Sh. Bilioni 6.7 za Kitanzania) baada ya timu hiyo kutwaa mataji matatu.

5. Bonasi ya uaminifu: Ili kuhamasisha wachezaji wakae klabuni kwa muda mrefu, klabu inaweza kutoa bonasi ya uaminifu ambayo hulipwa ambaye amechezea klabu kwa muda uliowekwa na klabu kwa mchezaji anayefikia kiwango hicho.

*Haki binafsi za mchezaji (image rights): Haki binafsi za wachezaji ni matumizi ya kibiashara ya vitu vya mchezaji kama jina lake, taswira na saini. Mara nyingi wachezaji huwa na mikataba tofauti ya haki hizi, ama kwenye klabu zao au kampuni. Haki hizi huweza kumuingizia mchezaji fedha nyingi kupitia mauzo kama ya bidhaa, matangazo na shughuli nyingine za kibiashara.

Kama ilivyoelezwa awali, ili kuweza kushbughulikia haki hizi kwa ufanisi, wachezaji huanzisha kampuni. Mfumo huu huwezesha wachezaji kupokea fedha kupitia kampuni hizo, ambazo hulazimika kulipa kodi kwa viwango vya kampuni (corporate tax) kuliko kulipa mwenyewe.

Viwango hivi huwa chini kuliko viwango vya kodi kwa mtu binafsi. Zaidi ya yote, wachezaji wanaweza kujilipa fedha na mgawo kutoka kampuni hiyo, kitu ambacho hupunguza zaidi mzigo wa kodi.

Mfano wa wachezaji na kampuni zao za haki binafsi:

1. Beki wa Man City, Joe Stones amevuna Pauni milioni 15 kutoka kampuni yake ya haki binafsi.

2. Mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial amekusanya Pauni milioni 8 kutoka kampuni yake ya haki binafsi

3. Paul Pogba ameendelea kuwa na kampuni yake ya haki binafsi nchini Uingereza ambayo ina mali zenye thamani ya Pauni milioni 5 za Kiingereza. Kuna uwezekano ana kampuni nyingine nchini Italia.

GHARAMA KATIKA SOKA LA KULIPWA

Wakati wachezaji hulipwa viwango vikubwa vya fedha, pia hulazimika kulipa gharama kubwa. Gharama hizo ni pamoja na:

*Ada ya wakala:Katika siku za hivi karibuni, Kanuni za Fifa za Mawakala wa Soka (FFAR) zimependekeza kiwango cha juu cha huduma za wakala wa soka kisivuke asilimia 5 ya mshahara wa mchezaji ambaye malipo yake ni chini ya Dola 200,000 za Kimarekani na asilimia 3 kwa mchezaji ambaye mshahara wake kwa mwaka hauzidi dola 200,000 za Kimarekani. Hata hivyo, viwango hivyo havitafanya kazi nchini England kutokana na hatua za kisheria kuendelea mahakamani. Mawakala hufanya kazi muhimu katika majadiliano ya mkataba na wakati mwingine huangaliwa kwa mtazamo hasi kwamba wanapata fedha nyingi kwa kazi ndogo, hilo si hivyo. Jukumu la wakala linakwenda mbali zaidi ya majadiliano ya mkataba.

*Kodi: Wachezaji wanatakiwa walipe kodi katika nchi wanazocheza, kitu ambacho hupunguza mapato yao. Viwango hutofautiana, lakini nchini Uingereza, kwa mfano, kiwango cha kodi ni asilimia 45 ya Malipo ya Kadiri Unavyopata (P.A.Y.E). Maana yake, mchezaji anayelipwa Pauni milioni moja agtakatwa kodi inayofikia Pauni 431,175.

Bima: Kumlinda na uwezekano wa kupata majeraha yanayoweza kukatisha kazi yake, mchezaji hukata bima inayoendana na hatari hiyo na hivyo huhusisha malipo makubwa.

Usimamizi wa fedha: Kutokana na mchanganyiko na ukubwa wa mapato yao, wachezaji huajiri washauri wa masuala ya kifedha kwa ajili ya kuweza kusimamia utajiri wao, uwekezaji na majukumu ya kikodi. Uimara katika usimamizi wa masuala ya kifedha huleta huimara wa kifedha wa muda mrefu, hasa kutokana na ukweli kwamba muda wa wachezaji kusakata soka la kulipwa ni mfupi.

Ni vipi washauri hao hulipwa, hutegemea na ukubwa wa suala lenyewe na nini hasa kinahitajiwa. Malipo kuwa naye (retainer), ya mara moja kwa mwaka, na mara nyingi kwa asilimia ya faida yanaweza kufanywa kwa mameneja wa masjuala ya kifedha ambao hupewa jukumu la kuingiza mapato kwa kutumia uwekezaji kwa niaba ya mchezaji .

Hii ni tafsiri ya Makala iliyoandikwa na David Skilling wa Original Football yenye kichwa kisemacho “Understanding The Income and Expenses of Club Football Contracts”, yaani ufafanuzi wa mapato na gharama za mikataba ya klabu za soka.

Chanzo: Mwanaspoti