Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Usajili mpya Yanga unashtua, Nabi akataa mastaa wa viongozi

Usajili Pic Data Usajili mpya Yanga unashtua, Nabi akataa mastaa wa viongozi

Thu, 8 Jul 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KOCHA wa Yanga, Nabi Nasreddine amesema usajili mpya wa timu hiyo utakuwa na utofauti mkubwa na uliozoeleka na hatapokea mchezaji yoyote wa kuletewa na kiongozi bila kujadiliwa kwa kina.

Mwanaspoti linajua Nabi tayari ameshapitisha usajili wa beki David Brayson wa KMC, Dickson Ambudo ambaye ni winga wa Dodoma Jiji na beki wa AS Vita, Djuma Shabaan ambaye jana picha zake akisaini mkataba zilikuwa zikisambaa mitandaoni.

“Nimekutana na uongozi tayari nimewaeleza chini yangu miongoni mwa mbinu ninayoitumia kupata wachezaji bora, sitaki kuona mchezaji ameletwa na kiongozi mmoja au mtu yeyote yule baada ya hapo anasajiliwa,” alisema Nabi ambaye kwenye mechi dhidi ya Simba wikiendi iliyopita alitumia fomesheni ya 4-2-3-1.

“Nataka iundwe kamati ya usajili ya watu wenye uweledi na masuala ya kiufundi nami nikiwemo humo, halafu katika kila eneo tunalohitaji mchezaji mpya kila mmoja wetu atakuwa na yule ambaye anataka asajiliwe.

“Hiyo kamati yetu ndio tutawajadili wachezaji hao kulingana na sifa alizokuwa nazo na mahitaji ya timu, yule atakayekuwa bora ndio tutamsajili, tofauti na hivyo hakuna mchezaji ambaye atasajiliwa.

“Sambamba na hilo nimewaambia viongozi kuna maskauti kutoka katika nchi mbalimbali Afrika na Ulaya ili kusaidiana nao katika masuala ya kiushauri na kupata wachezaji bora tutakaowahitaji,” aliongeza Nabi ambaye ana uraia wa Ubelgiji na Tunisia.

Nabi alisema miongoni mwa wachezaji anaowataka atakuwemo beki mpya wa kati mwenye uzoefu wa mashindano makubwa atakayekuja kuboresha eneo hilo akiunganisha nguvu ya pamoja na Dickson Job na Bakari Mwamnyeto ambao wanatumika zaidi wakati huu.

Alisema wakati huu ni mwanzo wa Yanga kurudi na kwenda juu kimafanikio kwa maana wanahitaji kuboresha kikosi chao ili kuwa na wachezaji ambao wana ubora na watakuja kutoa ushindani katika mashindano ya ndani na yale ya kimataifa.

Alisema amefundisha timu nyingi na anafahamu wachezaji wengi wazuri kama wale ambao wapo Al Merreikh lakini ni ngumu kupatikana kutokana na bajeti zao kuwa kubwa tofauti na hali halisi ya uchumi wa timu za Tanzania.

“Kuna wachezaji ambao nawafahamu kwenye ligi ya ndani wamefanya vizuri ila sina taarifa zao za kutosha lakini kwa kusaidiana na kamati ambayo nimetaka iundwe nadhani tutajadiliana na kupata waliokuwa bora,” alisema Nabi.

Katika hatua nyingine, Makamu Mwenyekiti wa kamati ya mashindano ya Yanga, Injinia Hersi Said alisema baada ya kuwafunga watani zao Simba wachezaji wao na benchi la ufundi watapata pesa nyingi kama bonasi ambayo haijawahi kutokea.

Hersi alisema Yanga wamejipanga zaidi kumpatia ushirikiano wa kutosha Nabi katika kila atakalokuwa anahitaji ili timu yao kuimarika na kuwa bora zaidi kama ambavyo kila mpenzi wa timu hiyo.

“Mipango yetu ni kuhakikisha tunakuwa na Yanga imara kuanzia kwa wachezaji mpaka maeneo mengine yote kulingana na mipango yetu uongozi hilo linawezekana,” alisema Hersi.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz