Mchambuzi wa soka Bongo, Master Tindwa amesema, usajili wa kipindi hiki cha mwezi disemba kwa maana ya dirisha dogo mara nyingi haulipi.
Amesema timu nyingi zinakuwa na mipango na wachezaji wake hivyo ni ngumu kupata mchezaji.
“Sajili kubwa kwa kipindi hiki nyingi huwa hazilipi, sasa hivi ligi zinaendelea mfano barani Afrika timu nyingi zipo kwenye makundi ya CAFCL na CAFCC wachezaji wengi wanye tija wapo huko na timu sio rahisi kuruhusu waondoke.
“Tanzania wachezaji wazuri wapo Azam ambayo inaongoza ligi na anatamani pengine kwa mwendo huu anaweza akapata ubingwa ni ngumu kukuuzia mchezaji wake.
“Situation kama hiyo ipo pia kwenye nchi zingine, kununua mchezaji ambaye wapo kwenye malengo ni nadra kwa sababu kupata mbadala wake ni ngumu,” alisema Master Tindwa.