Dirisha kubwa la usajili halijafungwa hadi Agosti 31, lakini wakati timu nyingi zikionekana kukamilisha zoezi hilo, utambulisho wa usajili wa winga Luis Miquissone ndio umeonekana kuteka hisia za wengi kwenye mtandao wa Instagram hadi sasa kuliko nyota mwingine yeyote aliyenaswa na timu ya Tanzania katika dirisha linaloendelea.
Winga huyo wa zamani wa Al Ahly ya Misri, utambulisho wa usajili wake, umepata idadi ya ‘likes’ 160,432 hadi wakati Arena napost taarifa hii, ukifuatiwa na ule wa mshambuliaji wa timu hiyo, Willy Onana ambao ulikuwa na ‘likes’ 119,277. Anayeshika nafasi ya tatu kiungo mpya wa Simba aliyenaswa kutoka Al Hilal ya Sudan ambaye utambulisho wake umepata idadi ya ‘likes’ 110,953 na anayemfuatia ni kipa mpya wa Simba, Jefferson Luis ambaye utambulisho wake katika mtandao huo wa Instagram umepata ‘likes’ 104,333.
Simba ni kama wametawala katika utambulisho huo wa wachezaji wao, kwani nyota wake tisa ndio vinara kwa kupata idadi kubwa ya ‘likes’ katika utambulisho wao, huku mmoja tu kutoka klabu nyingine ndiye akiingia katika nafasi moja iliyobakia ambayo ni ya 10.
Katika orodha hiyo, nafasi ya tano inashikiliwa na Aubin Kramo ambaye utambulisho wa usajili wake umepata ‘likes’ 97,397, Che Fondoh Malone yuko nafasi ya sita, akipata ‘likes’ 95,356 na aliyepo nafasi ya saba ni Shaban Iddi Chilunda ambaye amepata ‘likes’ 86,129. Nafasi ya nane inashikiliwa David Kameta ‘Duchu’ aliyepata ‘likes’ 77,087, Scudu Makubela wa Yanga yuko nafasi ya tisa akiwa na ‘likes’ 75,303 na anayefunga orodha hiyo ya 10 bora ni Gift Fred ambaye utambulisho wake una ‘likes’ 70,921 hadi sasa.