Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Urusi Washindwa Kesi Dhidi ya Vikwazo vya UEFA

Russia Nt Team Timu ya Taifa ya Urusi

Tue, 15 Mar 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha soka cha Urusi wataendelea kuzuiwa kushiriki michuano yote inayoendeshwa na Shirikisho la mpira Barani ulaya UEFA baada ya kushindwa kwenye kesi yao kwenye mahakama ya usuluhushi wa michezo {CAS}.

CAS hawakuona umuhimu wa kuweza kupindindua maamuzi yaliyowekwa na Shirikisho hilo huku ikiwa maamuzi yaliotolewa leo na mahakama hiyo yanahusu kwenye ushiriki wa michuano ya UEFA tu, kwa sasa Urusi wamebakiwa na tumaini moja kuhusu maamuzi ya FIFA ambayo hukumu yake bado haijatoka.

Wachezaji wa urusi na timu mbalimbali kutoka nchini humo zimezuiwa kushiriki mashindano yoyote na mashirikisho mbalimbali ya michezo Duniani na Ulaya, baada ya Serikali ya nchi hiyo kuivamia kijeshi nchi ya Ukraine.

Timu ya Taifa ya Urusi ilibidi imalize michezo yake ya kufuzu kombe la dunia mwezi huu lakini FIFA wamezipa ushindi timu zote ambazo zilipaswa kucheza na Urusi, huku timu pekee ambayo ilibaki kwenye mashindano ya ulaya Spartak Moscow nayo iliondolewa kwenye mashindano ya Europa League.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live