Hatua ya mchujo ya Ligi ya Europa inaendelea leo Februari 23 kwa mechi za marudiano hatua ya mtoano kufuzu 16 Bora.
Manchester United vs Barcelona (Agg 2-2) Uwanja :Old Trafford Muda 5:00 usiku
MECHI ZINGINE:
Muda saa 2:45 USIKU
PSV vs Sevilla (Agg 0-3)
Nantes vs Juventus (Agg 1-1)
Midtjylland vs Sporting (Agg 1-1)
Monaco vs Leverkusen (Agg 3-2)
Saa 5:00 USIKU
Union Berlin vs Ajax (Agg 0-0) Roma vs RB Salzburg (Agg 0-1) Rennes vs Shakhtar (Agg 1-2)
Baada ya sare ya 2-2 dimbani Spotify New Camp, Manchester United itakuwa mwenyeji wa FC Barcelona katika marudiano ya mchujo wa kufuzu hatua ya 16 ya #UEL.
Wakati Barcelona ikiwakosa Gavi (msururu wa kadi za njano) na Pedri (majeraha), Man United itawakaribisha Lisandro Martinez na Marcel Sabitzer ambao waliukosa mchezo wa kwanza kwa msururu wa kadi za njano.
Habari njema kwa mashabiki wa Manchester ni kwamba kiungo mkata umeme Carlos CASEMIRO leo anasherehekea siku yake ya kuzaliwa akitimiza miaka 31.
NB: Manchester United imeshinda mara moja tu mbele ya Barcelona katika Karne ya 21, nao ni ushindi wa 1-0 mnamo 2008 katika dimba la Old Trafford kupitia shuti la mbali la Paul Scholes ambalo liliipeleka United fainali baada ya sare ya 0-0 huko New Camp.
Manchester United ilitwaa ubingwa wa Ulaya katika fainali dhidi ya Chelsea kwenye matuta Mjini Moscow.