Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ureno walia na Mwamuzi kipigo dhidi ya Morocco

E33A81AF FF5A 407A 81B2 DAE2023BEBF2.jpeg Ureno walitupwa nje ya Michuano hiyo baada ya kukubali kichapo cha bao 1-0

Sun, 11 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki mtata wa Timu ya Taifa ya Ureno, Pepe ametupia lawama mamlaka zinazohusika na uandaaji wa Michuano ya Kombe la Dunia kwa kulaumu haikubaliki wachezeshwe na refa kutokea Argentina baada ya kutolewa na Morocco jana Desemba 10.

Ureno imetupwa nje ya michuano ya kombe la dunia katika hatua ya robo fainali na timu ya taifa ya Morocco kwa bao 1-0. Na ndipo mkongwe huyo akaibuka baada ya mchezo na kudai kua kilichotokea hawajakubaliana nacho hata kidogo.

“Haikubaliki kwa refa wa Kiargentina kuchezesha mchezo wetu, Nimehuzunika sana. Zilikua dakika 90 ambazo alitaka kusimamisha mchezo wetu kwa faulo ndogo ndogo na refa hakutoa kadi yeyote” Alisema Pepe Lima

Mkongwe huyo pia alienda mbali kwa kuona kua kama michuano hiyo imeandaliwa ili Argentina wawe mabingwa kwani ameeleza kuna vitendo alifanya Messi jana ambavyo si vya kiungwana lakini hakuna hatua yeyote ilichukuliwa na kusema wazi wawape Argentina tu kombe hilo.

Facundo Tello Muargentina ambaye alisimamia mchezo kati ya Ureno dhidi ya Morocco ikishuhudiwa Morocco wakiandika historia kwa taifa lao na bara la Afrika kwa ujumla amepata lawama kutoka kwa Pepe akidai alikua na lengo la kuhakikisha wanatoka kwenye michuano hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live