Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ureno haina makali Kombe la Dunia

Ureno Pic Ureno haina makali Kombe la Dunia

Fri, 18 Nov 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ureno ilishindwa kuvuka raundi ya 16 bora katika fainali za Kombe la Duna zilizofanyika mwaka 2006 kabla ya kutolewa tena raundi hiyo kwenye michuano ya Euro 2020. Ikafanikiwa kubeba ubingwa wa Euro mwaka 2016 katika fainali iliyocheza dhidi ya Ufaransa ambayo ilikuwa wenyeji wa michuano hiyo.

Vilevile Ureno ikabeba Ubingwa wa Nations League mwaka 2019 chini ya Kocha Fernandos Santos baada ya ushindi wa bao 1-0 ilipocheza dhidi ya Uholanzi.

Ureno imedumu na kocha huyo kutokana na mafanikio aliyowapa kwa mara nyingine atakiongoza kikosi hicho katika fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Qatar, kuanzia Novemba 20 mwezi huu aidha kocha huyo kibarua chake kinaweza kuota nyasi endapo atashindwa kufikisha Ureno mbali katika fainali za Kombe la Dunia Qatar.

Mara ya kwanza Ureno kushiriki fainali hizi ilikuwa mwaka 1966, kikosi chao kiliongozwa na mkali Eusebio ambaye ni marehemu kwasasa, ureno ikafanikiwa kushika nafasi ya tatu katika michuano hiyo. ureno ina rekodi ya kufuzu fainali Kombe la Dunia mara saba. Katika fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Russia, Ureno iliangukia raundi ya 16.

KWA NINI URENO

Nahodha wa Ureno, Cristiano Ronaldo ni mchezaji tegemeo katika kikosi kutokana na rekodi alizoweka kimataifa. Ameweka rekodi ya mfungaji bora kimataifa katika historia ya soka kwani amefunga jumla ya mabao 818 zaidi ya mchezaji yoyote hata hivyo hakuwahi kubeba ndoo ya Kombe la Dunia.

Wachezaji wengine muhimu wa kikosi cha Ureno ni Bruno Fernandes, Ruben Dias, Joao Cancelo, Bernardo Silva, Rafael Leao, Joao Felix, na Diogo Jota.

Mastaa hao wamekuwa na mchango mkubwa kuhakikisha Ureno inafanya vizuri katika mashindano yote wanayoshiriki, sasa wapo tayari kukiwasha Kombe la Dunia Qatar. Aidha Ureno itakosa huduma ya Jota baada ya kuumia kwenye ligi.

Chanzo: Mwanaspoti