Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Upo? Rice amenyoa kwa Sh77,000

Decline Rice Mnyoo Upo? Rice amenyoa kwa Sh77,000

Thu, 14 Mar 2024 Chanzo: Mwanaspoti

We huwa unanyoa kwa gharama ya kiasi gani. Kiungo ghali wa Arsenal, Declan Rice ameshtua watu baada ya kufichua gharama alizomlipa kinyozi aliyemnyoa kabla ya mechi ya FC Porto.

Kiungo huyo Mwingereza, mwenye umri wa miaka 25, alikuwa akizungumza na wachambuzi wa CBS Sports kabla ya mechi ya kumbukumbu ya kipekee kwa Arsenal katika usiku wa Ligi ya Mabingwa Ulaya huko Emirates.

Katika mahojiano hayo aliyofanyiwa na Kate Abdo, Thierry Henry, Jamie Carragher na Micah Richards, beki wa zamani wa Liverpool aliibua swali kwa kumuuliza Rice kuhusu mtindo wake alionyoa.

Carragher alisema: "Kabla hatujaanza, naona umenyoa maalumu kwa ajili ya hii mechi."

Rice alijibu: "Yeah usiku wa jana. Nipo tayari."

Abdo akauliza: "Unaweza kutuambia gharama yake? Hicho kitu tumekijadili sana hapa kwenye kipindi."

Hilo limetokana na kauli ya Richards alipowaambia wenzake kwamba inamgharimu Pauni 600 kwa wiki (zaidi ya Sh1.94 milioni) akinyoa mara tatu, kwa gharama za Pauni 200 sawa na Sh649,684.

Hiyo ni sawa na makadirio ya Pauni 24,000 kwa mwaka, yaani anatumia Sh77.9 milioni.

Lakini, Rice alisema: "Nadhani nililipa Pauni 24."

Kiasi hicho alichotaja Rice, kwa pesa ya Tanzania ni Sh77,962.1.

Carragher akamgeukia Richards na kumcheka, kitu kilichomfanya beki huyo wa zamani wa Manchester City, kumwambia Rice: "Kwanini unadanganya?"

Kiungo Rice alimjibu: "Ni kweli. Mimi naenda saluni. Simleti kinyozi nyumbani kwangu kama unavyofanya wewe."

Chanzo: Mwanaspoti