Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uongozi watoa tahadhari kwa wapinzani wa Namungo

Namungo Ilulu Namungo FC

Mon, 22 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Klabu ya Namungo umetoa tahadhari kuwa sasa mashabiki na wapenzi wa Soka wataanza kuiona Namungo haswa baada ya kumaliza michezo yao na Vigogo wa Soka wa nchi hili kwa raundi ya kwanza.

Akizungumza mara baada ya mchezo dhidi ya Yanga Meneja wa Namungo, John William , amesema

"Michezo yetu miwili iliyopita ilikuwa ni kujipanga dhidi ya Simba na Yanga, lakini tunashukuru tumemalizana nao na tumepata alama moja katika michezo hiyo miwili"

"Ila sasa kazi ndio kwanza inaanza, ni mwanzo wa kwenda kukusanya alama tatu kila mchezo, kwa hiyo ukiona unakutana na Namungo ujipange haitakua rahisi kwako" amesema

Namungo kwa sasa inakamata nafasi ya 11 ikiwa na alama Sita na ikiwa imeshacheza michezo sita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live