Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uongozi wa Yanga waweka wazi majukumu ya Chama

Gamondi Chama Dube Abuya 91021 Uongozi wa Yanga waweka wazi majukumu ya Chama

Thu, 18 Jul 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Uongozi wa Yanga umeweka wazi kuwa kiungo wao Clatous Chama amesema ana jambo lake ndani ya majukumu yake mapya msimu wa 2024/25.

Chama ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa Yanga ilikuwa Julai Mosi 2024 msimu wa 2023/24 alikuwa kwa watani zao wa jadi Simba.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa kiungo huyo amekabidhiwa jezi namba 17 kwa mpango kazi maalumu kuendelea kutimiza majukumu yake kwa umakini.

“Chama amekabidhiwa jezi namba 17 kutoka kwa Farid Mussa hii ni kazi nyingine kwake kwa ajili ya kutimiza majukumu yake na tunataka wale wasimsahau haraka wakimuona uwanjani.

“Chama ni yuleyule, uwezo wake ni uleule na amesema kuwa ana jambo lake hivyo ni jambo la kusubiria namna gani itakuwa kikubwa ni kuwa na subira.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live