Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

United yarejea baada ya Covid-19

Ralf Rangnick Man Utd F365 9 Meneja wa Man United, Ralf Rangnick

Thu, 23 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Manchester United Ralf Rangnick amesema wachezaji wake takribani wote wamerejea kwenye kikosi cha timu hiyo baada ya kushindwa kujiunga nayo kutokana na hofu ya maambukizi ya virusi vya Covid-19.

Kuibuka kwa kirusi kipya cha Omicron kulipelekea mechi mbili za Man United kuahirishwa, mtanange wa Brentford na ule wa Brighton.

Kuelekea mchezo wa Jumatatu dhidi ya Newcastle United Disemba 27, kocha Rangnick amesema atakosa huduma ya kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa Paul Pogba ambaye ni majeruhi.

“Leo ilikuwa ni siku ya tatu ya mazoezi, tulikuwa na wachezaji 25, ni Pogba pekee ambaye hakuwa sehemu ya mazoezi”. Alisema Rangnick

Chanzo: www.tanzaniaweb.live