Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

United yampa rekodi Klopp

Thumb 128301 Default News Size 5.jpeg Jurgen Klopp

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: Skysport

Baada ya kuibamiza Manchester United mabao 5-0, Jurgen Klopp amekuwa kocha wa kwanza kushinda mechi 200 ndani ya muda mfupi.

Katika mchezo huo uliochezwa Old Trafford jana, Liverpool ilikusanya pointi tatu kwa mabao ya Naby Keita, Diogo Jota na Mohamed Salah aliyeingia kambani mara tatu (hat-trick).

Huo ulikuwa ni ushindi wa 200 kwa Klopp katika mechi 331 pekee alizoiongoza timu hiyo tangu aajiriwe mwaka 2015 akitokea Bundesliga alikokuwa akiinoa Borussia Dortmund.

Aidha, Mjerumani huyo amekuwa kocha wa kwanza katika historia ya Liverpool kucheza mechi saba mfululizo bila kufungwa na Manchester United.

Chanzo: Skysport