Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

United iliongozwa na Carrick au Rangnick?

Carrick Michael Carrick, Kocha wa Muda Man United akitoa maelekezo kwa Ronaldo

Mon, 29 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Manchester United wamekataa utumwa wa kupokea idadi kubwa ya magoli toka Ole Gunnar Solksjaer ametimuliwa. Swali ni, timu ya wikiendi iliyopita ni Carrick au Rangnick?

Inafahamika kuwa ni suala la muda tu kabla Ralf Rangnick hajatangazwa kuwa kocha wa muda pale Old Trafford. Hii haina maana kuwa, Rangnick hajihusishi na United kwa sasa. Inawezekana, kocha huyu alikua anafatilia mchezo akiwa nyumbani au kuna namna alikua anawasiliana na waliopo kwenye benchi la ufundi la The Red Devils.

Zote ni hisia za mashabiki tu. Wengi walishangaa kumuona Cristiano Ronaldo akisugua benchi kwenye mchezo dhidi ya Chelsea, hakika, hata wapinzani walishangaa ni nini kimetokea. Aliamua Michael Carrick iwe vile au ni Ralf Rangnick alipanga kikosi?

The Red Devils walikua wakabaji kwa sehemu kubwa ya mchezo. Haijazoeleka huwa hivi kwa timu hii ambayo imejaa wachezaji wenye uwezo wa kushambulia. Pamoja na yote, uwezo wa David De Gea, umahisi wa McTominay, Matic na Fred kwenye safu ya kiungo, na mikimbio ya Sancho na Rashford, iliwapa afueni United ambao walifanikiwa kuondoka na pointi 1 pale Stamford Bridge.

Swali ni, Carrick ametuonjesha ladha ya timu itakavyokua chini ya Rangnick au mashabiki wa Manchester wategemee soka la namna gani msimu huu?

Chanzo: www.tanzaniaweb.live