Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unashangaa Sakho kwenda Ufaransa, siri iko hapa..!

Sakho Tizi 1.jpeg Pape Ousmane Sakho

Mon, 21 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa uzoefu wangu mchezaji anauzwa kutokana na vitu vikuu vitatu ambavyo ni vya msingi.

1. Kiwango chake (performance)

2. Ukubwa wa Taifa anakotoka.

3. Wasimamizi wake (agency)

Unaweza kuwa bonge la mchezaji lakini Taifa lako lisikuuze,unaweza kuwa na kiwango bora na umri mdogo lakini usiwe na wakala wa kukuuza.

Hapa Tanzania tuna wachezaji wengi wenye uwezo mkubwa na umri mdogo pengine kuliko Sakho lakini hawana watu sahihi wa kuwauza mfano Abdul Suleiman (Sopu)

Taifa nalo lichangia kwa asilimia kubwa kumpa thamani na uzito mchezaji hususa ni hawa vijana wetu kutoka hapa Africa.

Ukiwa na wachezaji wawili mmoja kutoka Senegal na mwingine kutoka Tanzania kisha ukawapeleka PSG lazima wa Senegal atapewa kipaumbele kutokana na ukubwa na historia ya taifa lake.

Pape Sakho anasimamiwa na Agency kubwa (wakala) iitwayo MDC ADVISORS.

Hawa jamaa wana connection kubwa barani Ulaya na kila siku wanazunguka barani Africa kutafuta vipaji na kuviuza Ulaya.

Mfano hivi majuzi wamewauza baadhi ya wachezaji kutoka Africa kwenda Ulaya kwa pesa ndefu mfano huyu kijana Abdoulie Sanyang,raia wa Gambia mwenye thamani ya €1.2m (tsh 3,251,224,080) ameuzwa Grenoble ya Ufaransa,Mamadou Diarra kwenda Grenoble ya Ufaransa mwenye thamani ya €1m (tsh 2,708,974,425) pia wapo wachezaji kibao wanaomilikiwa na hii Agency akiwemo Saidou Sow anayekipiga pale Saint Etienne na thamani yake ni (tsh 7bn) bila kumsahau Aziz ki wa Yanga.

Pamoja na Sakho kupoteza namba ya kudumu kwenye kikosi cha Simba lakini wakala wake alianza kufanya mipango ya nyota huyo kuitwa kwenye timu ya taifa ya Senegal kwani alijua hii itampandisha thamani mteja wake kisha akavigonganisha vilabu vya Grenoble na Quevilly-Rouen Métropole kutaka saini yake kwa wakati mmoja.

Mwisho wa siku imetoka $850,000 Sakho amejiunga na Quevilly-Rouen Métropole.

Guys mpira ni akili,mpira ni biashara, mpira ni Connection msibishe Sakho kununuliwa Bilioni 2.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live