Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unapovaa jezi ya timu yako fahamu hiyo sio nguo tu, bali ni historia

Pacome Yanga Cr Pacome Zouzoua.

Fri, 1 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Unapovaa jezi ya timu yako fahamu hiyo sio nguo tu bali ni historia, ni hisia na juu ya yote ni maisha ya watu, ni rahisi kusikia Mtu amefariki baada ya Yanga au Simba kupoteza kwakuwa ni sehemu ya maisha yao hizi timu.

Nakumbuka kabla ya fainali ya UEFA 2012 kati ya Chelsea na Bayern Munich, wachezaji wote baada ya kuvaa jezi akasimama Daktari wa timu Mhispania Paco Biosca, pembeni yake alikuwa Eva Carneiro (Daktari wa timu ya kwanza) na Jose Mario Rocha Mtalaam wa Utimamu, Biosca akasema:

“As doctors, we are not trained to communicate and understand the power of our words as it is related to patient’s ability and desire to survive” hapo alimnukuu Mtalaam Bernie Siegel! Maana yake ni kuwa wao Madaktari hawakwenda shuleni kufundishwa namna ya kumpa maneno ya matumaini mgonjwa bali ni utayari wa mgonjwa kuwa tayari kuwa hai, ukurasa ukafungwa watu wakaenda kubeba UEFA.

Hata leo hii Wachezaji wote wa Yanga wanapaswa kufahamu hakuna idadi ya Mashabiki wala ukubwa wa posho utakaofanya washinde mechi bali dhamira ya kweli kutoka moyoni kuwa wanashinda mechi, kuamini ni kushinda, wanapaswa kubaki na imaani thabiti kuwa wanashinda mechi hii.

Ni usiku mwingine tena wa kuitetea klabu hii yenye mchango mkubwa kwenye uhuru wa Tanganyika na ustawi wa Muungano, Karume alitoa majengo, Kaunda akawapa kiwanja na sasa ni zamu yenu kuwapa furaha Wananchi, inawezekana mkiamini tu! Jioni hii Mizimu ya Wanyakyusa kutoka Ziwa Ngosi ipo nanyi, Chemchem za Oldonyo Lengai Kaskazini mwa Tanzania pamoja nanyi na bendera inapaswa kupepea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live