Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unaikumbuka Yanga ya Bakuli? Acha Wananchi watambe

Tano Ta Yanga Unaikumbuka Yanga ya Bakuli? Acha Wananchi watambe

Tue, 12 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tatizo la mashabiki wa mpira wanapenda kuvisikia vitu wavipendavyo wao, mfano ukiongelea ubora walionao Yanga SC utaanbiwa sijui wewe ni Mnyama.

Ngoja niwakumbushe jambo. Viongozi wa Yanga walipopitia kwenye uchungu wa zaidi ya misimu minne siyo kwamba walilala na kupata usingizi, jibu ni hapana walikesha kutaka kujua walikosea wapi.

Hivi mmesahau yale maumivu waliyoyabeba kipindi kile cha BAKULI vipi leo wakitesa kwa haya maboresho yao. Kama wewe jirani utachukizwa na nini ndugu yako alipoamua kufanyia kazi.

Si ndo sisi ambao tulikuwa tukisisitiza Viongozi kuiga mfano kutoka kwenye uongozi bora chini ya Mo Dejwi. Vipi leo tumeshasahau.

Kama uongozi wa Yanga unamefuata taratibu zote na timu imesheeni wachezaji wenye uwezo vipi leo tuseme ni hujuma, inamaana tunaukataa ubora wa Diarra, tunapingana na usajli wa beki kitasa Ibrahim Baka, vipi Stephanie Aziz Ki, au Pacome Zouzou.

Ndugu zangu nikiiandikia sana Yanga hamtachelewa kuniita hayo majina yenu ila ukweli ni kwamba, Yanga SC wamejipata mimi hata sina shaka na ubora wao.

Kitendo kile cha Simba SC kupoteza Kwa idadi kubwa ya mabao tena goli 5-1 ile ilikuwa ni ishara kwamba Yanga SC imedhamiria kuifunga timu yoyote ile siyo tu hapa hata huko kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Vipi nimemsahau Maxi Nzengeli, hahahah jamani mtuelewe tu Yanga imejipata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live