Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unaijua siri iliyopo nyuma ya Tuzo za Ballon D'or?

 121855517 Witfaithandannetterememberdinigerianwomanweydiemysteriouslyforcted'ivoireprison.jpeg Unaijua siri iliyopo nyuma ya Tuzo za Ballon D'or?

Fri, 3 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lionel Messi ameshinda tuzo yake ya nane ya Ballon d'Or na kuweka rekodi ambayo wanaokuja watapata tabu sana kuikaribia...achilia mbali kuifikia au kuivunja.

Tangu 2008, Ballon d'Or imekuwa ikitawaliwa na wachezaji wawili, Lionel Messi na Cristiano Ronaldo, na katika kipindi hicho hakuna kigezo chochote kilichowahi kujulikana, zaidi ya kusema walikuwa bora sana!

Kabla ya hapo, mafanikio binafsi ya mchezaji na timu yake kwenye kushinda mashindano makubwa vilikuwa vigezo namba moja.

Lakini tangu Messi na Ronaldo waingie, vigezo vimekuwa wao wenyewe tu, siyo kushinda mashindano.

Kwa mfano, mwaka huu Messi amefaidika na mafanikio yake akiwa na timu ya taifa, Argentina, kwa kushinda Kombe la Dunia.

Lakini hata hivyo, ushindi wa Kombe la Dunia haukuwahi kuwa kigezo katika miaka yote pale Messi na Ronaldo walipokuwa wakishinda tuzo hii.

2010 - Messi

Messi alimaliza bila hata bao moja, huku timu yake ikidhalilishwa na Ujerumani kwenye robo fainali kwa kichapo cha 4-0.

Diego Forlan wa Uruguay alimaliza kama mchezaji bora wa mashindano pia akiwa mfungaji bora mwenza, akilingana na Wesley Schneider wa Uholanzi.

Forlan aliiongoza Uruguay kufika nusu fainali na Schneider akaifikisha Uholanzi fainali.

Zaidi ya hapo, Schneider aliiongoza Klabu ya Inter Milan kushinda Treble, Ligi ya Mabingwa Ulaya, Serie A na Kombe la Italia.

Kwenye Ligi ya Mabingwa, waliitoa Barcelona ya Messi huku Schneider akifunga moja ya mabao ya ushindi.

Andreas Iniesta aliiongoza Hispania kushinda Kombe la Dunia, akifunga bao la ushindi na kupata tuzo tatu za mchezaji bora wa mechi, katika mechi saba za mashindano, ikiwmeo fainali yenyewe.

Messi aliiongoza Barcelona kushinda ligi ya Hispania pekee, lakini hiyo ikatosha kumfaya ashinde Ballon d'Or.

Kigezo kikawa La Liga..siyo Kombe la Dunia wala Ligi ya Mabingwa.

Mwaka 2012, Cristiano Ronaldo akiwa Real Madrid, alifunga mawili dhidi ya Granada kwenye mchezo wa La Liga.

Hakushangilia hata bao moja na kipindi cha pili akaomba kufanyiwa mabadiliko baada ya kuumia

Mwisho wa mchezo, akahojiwa na waandishi kwanini hakushangilia mabao yake, akajibu kwa sababu ana huzuni.

"???? ????????????'???? ???????????????????????????????????? ???????????????????? ???????????????? ???? ???????? ???????????????????????????? ???????????? ???????????? ????????????????'???? ???????????? ???????????????? ????????????????????.

???????????? ???????????????????????? ???????????? ???????????????? ???????????????? ???????????????? ???????????? ???????????? ???? ????????????'???? ???????????? ???????????? ???????????????? ???????????????? ????????????????."

???????????????????????????????????????????? ???????????????????? ???????????????? ???????????????????????????????????????? ???????? ???????????????????????? ???????? ???????????????????? ???????????????????????? ???????????????????????????????????????????????? ????????????.

???????????????? ???????????????????????????????????????? ???????????????? ???????????????? ???????????????????????????? ???????????????????????????? ???????? ???????????????????????????????? ???????????????????? ???????? ????????????????.

Cristiano alijiunga na Real Madrid mwaka 2009 kwa mkataba wa miaka sita.

Hadi 2012 alikuwa tayari amemaliza miaka mitatu, anautafuta wa nne.

Mazungumzo ya mkataba mpya yalishaanza lakini yalisimama.

Kwa hiyo kauli ile ikaibua hisia kwamba yawezekana Ronaldo ana huzuni kwa sababu ya fedha kwenye mkataba mpya.

Akatoa ufafanuzi baadaye kwamba tatizo kwake siyo pesa.

"????'???? ???????????? ???????????????????? ???? ???????????????????????????????????????????????? ????????????????????."

???????????????? ???????????????????????? ???????????? ???????????????????????? ???????? ???????????????????? ???????? ????????????????????????????????.

Gazeti la Marca ambalo huandika zaidi habari za Real Madrid, likachunguza huzuni ya Ronaldo na kuja na taatifa ifuatayo.

Mojawapo ya makubaliano ya Ronaldo na Florentino Perez wakati wa uhamisho kutoka Manchester United ilikuwa kumsaidia kushinda Ballon d'Or.

Lakini hakushinda 2009, 2010 na 2011 na hadi hapo tuzo za 2012 zilikuwa zinakaribia na Ronaldo hakuona kama anaweza kushinda.

Kwa hiyo kwenye mazungumzo ya mkataba mpya akawa hataki hadi Perez atoe ahadi kwamba sasa atafanikisho hilo.

Lakini Perez akawa anasita, mazungumzo ya mkataba yakakwama...Ronaldo akawa na huzuni.

Kwenye tuzo za 2012 alialikwa lakini hakwenda na akasema hatoenda tena.

Lakini mwaka 2013 Ronaldo na Real Madrid wakafikia makubaliano ya mkataba mpya na kwenye Ballon d'Or za 2013 akaenda...na akashinda!

Chanzo: www.tanzaniaweb.live