Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unai ajibu aonyesha ubabe EPL

Unai Emery.jpeg Kocha wa Aston Villa, Unai Emery

Fri, 17 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Nyota wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher alisema baada ya makocha Jurgen Klopp na Pep Guardiola, anayefuatia kwa ubora ni Unai Emery wa Aston Villa.

Sasa katika kuthibitisha hilo, ni alichokifanya Unai baada ya kuiwezesha Villa kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu ujao ikiwa ni baada ya miaka 41 mara ya mwisho timu hiyo kufuzu.

Villa imejihakikishia kumaliza ndani ya top four na ina pointi 68 kabla ya mchezo wa mwisho Jumapili, Mei 19 kumaliza msimu wa 2023/24.

Pointi hizo 68 ilizonazo haziwezi kufikiwa na timu inayoifuata, Tottenham yenye 63 na ikishinda mchezo wa mwisho itafikisha 66.

Unai alijiunga na Villa Oktoba 2022 na aliikuta timu ikiwa nafasi za chini kabla ya kuiwezesha kupanda na kumaliza ya saba kwenye msimamo wa ligi msimu huo na kucheza michuano ya ulaya ya ya saba , alipoikuta timu ikiwa nafasi za chini na kuiwezesha kumaliza nafasi saba za juu na ikafuzu kucheza michuano ya Ulaya ya Europa Conference League ilikofika nusu fainali msimu huu.

Tangu ajiunge na Villa, Emery ameshinda asilimia 57 ya mechi zote za Ligi Kuu England hali iliyomfanya kuwa kocha wa kwanza kushinda mechi nyingi zaidi ndani ya muda mfupi baada ya John Gregory (asilimia 41) na Martin O’Neill (asilimia 40) .

“Tumekuwa tukizungumza kuhusu Klopp na Guardiola ni makocha bora duniani, kwangu mimi Emery ndiye bora ajaye kwa EPL.”

“Nasema ni bora kutokana na mafanikio yake, Arteta anafanya vizuri lakini huyu jamaa ameshinda hadi Europa League, pia ametembea na kushinda mataji sehemu mbalimbali.”

Mara ya mwisho kwa Villa kushiriki Ligi ya Mabingwa ni mwaka 1982–83 wakati huo ikiitwa European Cup na ilifuzu kama bingwa mtetezi baada ya kuchukua msimu wa 1981–82.

Chanzo: Mwanaspoti