Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unai Emery kwenye rada za New Castle

U1 Unai Emery

Tue, 2 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa klabu ya soka Villareal, Unai Emery anaongoza mbio za kuwania nafasi ya kuwa kocha kwenye timu ya Newcastle United ambao hawana budi kulipa kiasi cha Euro Milioni 5, kwa mabingwa wa Europa kama gharama za kuvunja mkataba wake.

Mazungumzo yamefanyika kati ya Emery na uongozi wa klabu ya Magpies katika muda wa saa 48 zilizopita huku makubaliano yakitarajiwa kukamilishwa siku ya Jumatano.

Wamiliki wapya wa Newcastle wana nia ya kubadili matokeo ya klabu hiyo baada ya kuanza bila ushindi msimu huu, wakiwa nafasi ya pili kutoka mwisho kwenye msimamo wa Ligi Kuu ya Uingereza na pointi sita.

Chanzo cha karibu na kocha wa zamani wa AS Roma, Paulo Fonseca kimeweka wazi kwamba, kwa hali ilivyo, hakuna uwezekano Mreno huyo kuteuliwa kuwa mrithi wa Steve Bruce aliyetimuliwa hivi karibuni, kama taaraifa za mwanzo zilivyokuwa zisema.

Ikumbukwe Unai aliwahi kuifundisha Sevilla kwa mafanikio makubwa alipoisaidia kutwaa taji la Europa mara tatu mfululizo kabla ya kujiunga na matajiri wa Ufaransa, PSG na baadae kutimkia kwa washika mitutu wa Arsenal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live