Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unai Emery aiweka mtegoni Aston Villa

Unai Emery X Villa.png Unai Emery aiweka mtegoni Aston Villa

Mon, 6 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Aston Villa imeonywa kuishi kwa akili kwa sababu kocha wao Unai Emery atapewa dili la maana na klabu inayoshiiki Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya, na hatalikataa, atakwenda na kuwaacha.

Hayo ni maneno ya beki wa zamani wa Liverpool, Jamie Carragher akidai kwamba anachofanya Mhispaniola huyo kwenye kikosi hicho cha Villa Park kinampa nafasi kubwa ya kuchukuliwa na timu kubwa zaidi.

Mavitu ya Emery huko Villa Park ni balaa kubwa, ambapo ni Manchester City, Arseal na Liverpool ndizo zilizoshinda alama nyingi kwenye Ligi Kuu Engand kuzidi Aston Villa tangu kocha huyo alipojiunga nao Novemba 2022.

Carragher alidai pia kocha huyo wa zamani wa Villarreal bado ana biashara zake hajazimaliza kwenye timu kubwa baada ya kuwahi kupita kwenye timu za Paris Saint-Germain na Arsenal.

Na madai ya beki huyo wa zamani wa England tayari atakuwa kwenye orodha ya makocha wanaosakwa na timu kubwa.

Carra mwenye umri wa miaka 45, alisema: Aston Villa wanapaswa kumshukuru Unai Emery kwa kadri wanavyoweza. Ni suala la muda tu kabla ya kocha huyo hajaletewa ofa tamu na klabu za Ligi ya Mabingwa Ulaya, ambayo hataweza kuigomea.”

Emery alishinda taji la Europa League mara tatu alipokuwa na kikosi cha Sevilla na mara moja akiwa na Villarreal na aliongoza PSG kushinda ubingwa wa Ligue I alipokuwa kwenye kikosi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live