Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Unai Emery abeba matumain ya Mashabiki Aston Villa

Unai Emery Aston Villa Unai Emery

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Yeyote anayehofia kama Unai Emery anaweza kuifufua Aston Villa anapaswa kuelewa itakuwa rahisi ikilinganishwa na kile alichokabiliana nacho kama meneja mchanga huko Valencia.

Mhispania huyo, aliyefikisha umri wa miaka 51 siku ya Alhamisi, anawasili Villa Park na timu iliyo juu ya eneo la kushushwa daraja ikiwa na pointi moja.

Wameshinda mechi tatu pekee msimu huu na wana mapungufu makubwa kwenye maeneo yote ya uwanja.

‘Changamoto kubwa mbele,’ ilisomeka tweet kutoka kwenye akaunti rasmi ya Emery Jumatano asubuhi.

Emery anarudi kwa mara ya pili EPL akichukua mikoba ya Steven Gerrard alieoneshwa malango wa kutokea.

Awali Unai aliwahi kukonoa kikosi cha Arsenal kabla ya kutimkia Hispania ambako alifanya vyema na Sevilla.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live