Baada ya kuchezea kichapo cha 4-2 kutoka kwa Olympiakos ya Ugiriki, Meneja wa Aston Villa Unai Emery, hakusita kuweka wazi namna alivyochukizwa na kuumizwa na matokeo hayo.
Aston Villa ilipoteza mchezo wa Mkondo wa Kwanza wa Nusu Fainali wa michuano ya Europa Conference League uliopiga usiku wa kuakia leo katika Uwanja wa Villa Park.
Kocha huyo kutoka nchini Hispania amesema amesikitishwa sana na matokeo hayo ambayo yanawapa wakati mgumu kuelekea kwenye mchezo wa Mkondo wa Pili utakaopigwa juma lijalo kwenye Uwanja wa Georgios Karaiskakis nchini Ugiriki.
“Nimechanganyikiwa, nimechanganyikiwa sana, lakini lazima nikubali,” Emery alisema baada ya mchezo.
“Hatukucheza vizuri. Tulijiandaa kushinda katika Uwanja wa nyumbani, lakini haijawa bahati kwetu kushinda.
“Tumepoteza. Ninakubali tumepoteza lakini katika mchezo huu tumepoteza katika wakati muhimu wa kupata kitu muhimu katika michuano hii ya Uropa, tulipoteza nafasi nzuri.
“Tulistahili kupoteza na wapinzani wetu walistahili kushinda. Tutajaribu kupambana katika mchezo wa mkondo wa pili, ninaamini tunaweza kufanya kitu ugenini.
“Tuna mchezo ya Ligi Kuu dhdii ya Brighton na ni muhimu sana Jumapili. Kama kawaida, katika mechi 38 ndio muhimu zaidi kwa sababu ni mahali ambapo unaweza kuhisi nguvu katika mechi 38 kuwa thabiti.
“Tunapata lengo letu la kwanza kupitia hilo. Bila shaka, tunapoingia nusu fainali ni fursa nzuri sana. Tulikuwa tukihangaika sana dhidi ya Lille na tukashinda raundi hiyo mwishoni kwenye mikwaju ya Penati.
“Tunahitaji utulivu na kupata changamoto mpya katika mchezo wa Mkondo wa Pili. Tunacheza huko Brighton Jumapili na ni lengo letu 100%.