Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umemwona nani pichani?

Djuma Shaban Azam FC.jpeg Aliyekuwa Mlinzi wa Yanga Djuma Shaban akiwa mazoezini na Kikosi cha Azam FC

Wed, 6 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakati ikionekana kuwa Uhamisho wake kujiunga na Azam FC ulikwama dakika za lala salama, aliyekuwa Mlinzi wa Yanga Mcongo Djuma Shaban bado yupo katika kikosi cha Matajiri hao wa Jiji.

Taarifa kutoka katika chazo cha kuaminika zinasema mchezaji huyo anajifua na kikosi cha Azam ili kujiweka fiti na iwapo atawavutia mabosi kwa kiwango chake basi atajiunga nao Dirisha dogo.

"Ni kweli Shaban Djuma yupo kwenye viunga vya Azam akifanya mazoezi tu kama mchezaji mwalikwa , kwa sasa timu imekamilisha wachezaji 12 kimataifa kama kanuni inavyotaka kama kutakuwa na suala la usajili wake basi ni wakati wa dirisha dogo" Alisema mtoa taarifa

Chanzo: www.tanzaniaweb.live