Mechi ya Ligi Daraja la Nne England (League Two) kati ya Gillingham na Wimbledon ilisimamishwa kwa muda kutokana na hitilafu ya umeme.
Hitilafu ya umeme ilitokea katika dakika ya 64 wakati kukiwa hakuna bao katika mchezo huo wa Ligi Daraja la Nne.
Ilibidi vikosi vya timu zote mbili kutoka nje ya uwanja, kabla ya Gillingham kuthibitisha sababu ya suala hilo ni kutokana na kukatika kwa umeme katika eneo hilo.
Waliandika kwenye Twitter: “Vema, tumekuwa hapa hapo awali ....
“Taa zimezimika! Wachezaji wanarudi kwenye eneo la chumba cha kubadilishia nguo.
“Tunaelewa kuwa umeme umekatika katika eneo la karibu. Tutakufahamisha, huenda tukasubiri kwa muda mfupi.”
Usumbufu huo ulisababisha mashabiki wa Wimbledon waliokuwa wakisafiri kuikejeli Gillingham walipokuwa wakisubiri mchezo kurejea ndani ya Priestfield.
Walisikika wakiimba: “Huwezi kulipa bili zako.”
Na mtandao wa kijamii wa Wimbledon ulikiri uimbaji huku wakichapisha: “Wachezaji wanaondoka uwanjani kwa sasa na kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo. Hiki hakikuwa kile tulichopanga!
“Mashabiki wa Dons wanafurahia gizani kwa sauti.”
Mwaga wa taa ulirejea baada ya dakika 16. Wachezaji walipewa nyongeza ya dakika tano kabla ya mchezo huo kuanza tena. Hata hivyo, Gillingham iliibuka na ushindi wa bao 1-0 shukrani kwa Conor Masterson aliyefanya yake katika dakika 85.