Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umeiona Azam! usajili mpya sasa washtua

Azam FC FC Azam inafanya usajili kila kunapokucha

Thu, 14 Jul 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Kama kuna kitu Simba na Yanga wanatakiwa wajipange nacho msimu huu, ni hii habari ya Yusuf Bakhresa. Mmoja wa wana bodi ya Azam FC kwenda mstari wa mbele katika kusimamia timu.

Yusuf hana(ga) shughuli ndogo. Anaujua mpira na anajua njia zote za kupita kwenye mpira. Kabla sijaanza kumuelezea kiundani, nikutonye sikio kwamba msimu ambao Azam FC ilikuwa bingwa wa Ligi Kuu, 2013/14, Yusuf Bakhresa alikuwa mstari wa mbele kama anavyoonesha sasa.

Tena safari hii kapiga hatua moja mbele, anaonekana hadi kwenye picha za utambulisho wa wachezaji. Angalia hiyo picha hapo. Wakati ule hakuwa akionekana kwenye picha.

NI NANI HUYU YUSUF BAKHRESA

Ni mtoto wa nne wa bilionea mzawa, Said Salim Bakhresa, mwanzilishi wa kundi la kampuni za SSB chini ya jina chapa la Azam.

Msomi wa biashara na fedha kutoka Chuo Kikuu cha Portsmouth Uingereza, Yusuf Bakhresa alizaliwa Mei 7, 1983 jijini Dar es Salaam na maisha yake makubwa ameyaishi kwenye mpira.

Ni mmoja kati ya Watanzania wa kwanza kabisa kupata leseni ya FIFA, kuwa mawakala.

Mwaka 1998, yeye ndiye aliyewapeleka Sweden kwenye mashindano maarufu ya Tivoli, vijana wa Kitanzania kama kina Juma Kaseja, Shekhan Rashid, Athuman Machupa, nk.

Tangu hapo amekuwa akijihusisha na mpira wa nje na wa ndani hadi walipoamua kuanzisha klabu yao hii ya Azam FC. Baada ya maanguko kadhaa ya klabu hiyo chini ya watu waliowaamini, sasa Yusuf Bakhresa anaenda kuongeza nguvu kwa watu hao ili kuipeleka juu zaidi klabu hiyo.

AMEANZA NA USAJILI

Hadi sasa Azam FC imeshusha vyuma vitatu kutoka nje, na inasemekana kuna vingine vitatu vinakuja.

KIPRE JUNIOR

Huyu ni winga teleza kutoka Ivory Coast, mji ule ule anaotoka Kipre Tchetche, winga wa zamani wa klabu hiyo aliyeacha alama kubwa Chamazi. Tangu aondoke 2016, Kipre Tchetche amekuwa na uhusiano mazuri na Yusuf na ndiye aliyemtambulisha kwa Kipre Junior.

Haikuwa kazi kubwa, Tchetche alimwambia Yusuf kwamba Kipre Junior ni zaidi yangu.

Katika ligi ya msimu huu, Kipre Junior amefunga mabao 5 na kutoa pasi 10 za mabao.

Takwimu hizo pamoja na vitu vingine ambavyo haviwezi kuwekwa kwenye takwimu, vikamfanya awemo kwenye kikosi bora cha Ivory Coast cha 2021/22.

Akiwa na miaka 22, Kipre Junior ambaye jina lake halisi ni Kipre Junior Emmanuel Zunon, amekulia kwenye akademi ya Asec Mimosas ya Ivory Coast na baadaye akaenda kwenye akademi ya Strasbourg ya Ufaransa.

Ili kufanikisha dili lake, Yusuf alimpanga mama mzazi wa mchezaji huyo kwa sababu mawakala wake na hata klabu yake ya FC Sol, ilikuwa inataka aende TP Mazembe.

TAPE EDINHO

Kama kuna mtu kaja kuwasahaulisha Watanzania kuhusu Clatous Chama, basi ni Tape Edinho.

Huyu jamaa ni namba 10 wa kiwango cha juu sana. Akiwa na umri wa miaka 19, msimu ulioisha akiwa na klabu yake ya ES Bafing, ameingia kwenye kikosi bora cha Ligi Kuu ya Ivory Coast.

Alifunga mabao 5 na kutoa pasi 9 za mabao. Klabu ya Asec ilimtazama huyu kama mrithi sahihi wa Aziz Ki ambaye alishambuliana na klabu hiyo kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu.

Lakini Edinho mwenyewe aliikataa Asec kwa sababu alikuwa aende Ufaransa, ila Yusuf Bakhresa akaingilia kati na kutoa dau kubwa pamoja na makubaliano mengine maalumu...Tape Edinho akatua Chamazi.

ISSAH NDALA

Watanzania wanamfahamu sana Issah Ndala baada ya kumuona akiwa na klabu yake ya Plateau United alipokuja kucheza na Simba SC, Disemba 2020.

Alikichafua sana pale kati na kuwapoteza viungo wa Simba.

Baada ya hapo alienda Armenia kwa mkopo kwenye klabu ya Saven FC ambayo ilipanda daraja.

Lakini mambo hayakuenda vizuri baina ya klabu hiyo na Plateau United hivyo akarudi Nigeria na Yusuf Bakhresa akapita naye.

Ndala ni mchezaji mwenye umri mdogo wa miaka 19 lakini ana uzoefu mkubwa kutokana na kuanza kucheza soka katika umri mdogo zaidi.

NA BADO

Yusuf Bakhresa anasema hajamaliza kushusha vitu. Anataka kumshusha kipa na beki wa kati ili kuimarisha safu ya ulinzi, na kushusha kiungo wa ushambuliaji ili kukamilisha usajili wa kigeni kwenye dirisha hili.

Wawili, beki wa kati na kipa, wanatoka nchi mmoja, kwenye ligi iliyoendelea ambayo inaweza kutoa mchezaji moja kwa moja akacheza England.

Kiungo wa ushambuliaji naye anatoka katika nchi yenye sifa hizo, ambayo ni jirani na ya wale wawili wa juu.

Wachezaji hao wanacheza timu kubwa ya taifa ya nchi zao, ambayo kwa asilimia kubwa inaundwa na wachezaji wanaochezea Ulaya.

SASA PATA PICHA

Hebu iangalie ile Azam FC ya kwenye Mapinduzi Cup na soka lake ililokuwa ikilitandaza.Umeshawahi kuwaza kwanini ghafla ikawa haichezi vile tena?

Kucheza soka kama lile halihitaji wachezaji wanaojitahidi bali wanaojua.

Wachezaji wanaojitahidi huweza kufanya vile kwa muda mfupi sana, na ndiyo maana baada ya Mapinduzi, Azam FC ikashindwa kuendeleza moto ule.

Ndiyo maana Azam FC wenyewe wameamua kubaki na yule kocha wakiwa na imani kwamba mbinu zake ni sahihi na soka lake ni zuri sana kulitazama...lakini tatizo alikosa watu sahihi wenye kujua badala ya kujitahidi.

Safi ya kiungo kule kwenye Mapinduzi Cup iliundwa na Kenneth Muguna kama kiungo wa chini. Frank Domayo kama kiungo wa juu na Ibrahim Ajib kama kiungo mchezesha timu yaani namba kumi.

Muguna ameendelea kubaki na kiwango chake kwa sababu anajua, lakini Domayo na Ajib ambao walikuwa wanajitahidi, wakapotea na nafasi zao kuchukuliwa na Mudathir Yahya na Prince Dube.

Mudathir akamtoa Domayo na kupotea kwa Ajib kukamlazimisha mwalimu kumtumia Dube ili acheze pacha Rodger Kola kama Sopu

Chanzo: Mwanaspoti