Ni wakati Sasa viongozi wa nchini Tanzania kuongoza soka Kwa muda mrefu.
Achana na Siasa za nchi njoo kwenye siasa za mpira, ambapo huku viongozi huongoza Kwa muda wa miaka minne baada ya hapo wanakuwa na muda wa kuongoza muhula wa pili Ili watimize miaka 8 baada ya hapo kiongozi anakuwa hana nafasi ya kuongoza tena katika nafasi hiyo kama sheria inavyoeleza.
Kwenye maisha ya soka ni tofauti kabisa na siasa nyingine, huku Kuna mipango ya muda mrefu na muda mfupi, Ile ya muda mfupi inaweza Kuchukua mwaka mmoja hadi mitano lakini mipango ya muda mrefu inaweza Kuchukua mpaka miaka 10.
Morocco hii tunayoiona imepiga hatua katika soka la taifa na klabu ni Kwa ajili ya mipango madhubuti waliyoiweka na kuindaa tangu 1980s.
Klabu zinazoendeshwa na wanachama mfano Barcelona na Real Madrid marais wao wanadumu Kwa muda mrefu ndiyo maana tunaona wanatawala soka la Ulaya Kila iitwapo Leo
Mfano Joan Laporta ameiongoza Barca tangu 2003 mpaka Sasa licha ya kupumzika 2010 alipokuwa anafanya shughuli za siasa
Lakini Florentino Perez yeye yupo Madrid tangu 2000 na ndiyo Klabu iliyobeba Mataji mengi kuliko Klabu yeyote barani Ulaya.
Tugeuke Kwa FIFA ambaye ndiyo baba wa mpira rais wa 51 Jossep Blatter aliongoza Kwa zaidi ya miaka 15 baada ya Kuchukua nafasi ya Havelange aliyeongoza FIFA 1974-1998.
Unaweza kuona ni kwanamna gani Ili mpira uendelee inahitaji kiongozi ahudumu Kwa muda mrefu Ili asimamie maono yake na kuyatekeleza.
Niwakati Sasa soka la Tanzania kubadilika katika maono.
Lakini pia wakati nazungumza Kwa wenzetu waliotutangulia msisahau sifa ya kiongozi wa mpira anatakiwa kuwa na hela.
Ameandika James TupTupa.