Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Umakini haukwepi muda wa mavuno

Yanga XNMB.jpeg Umakini haukwepi muda wa mavuno

Wed, 12 Jul 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mavuno yanaongeza tabasamu hasa kila kitu kinapokwenda sawa ila inapokuwa tofauti hakuna ambaye anapata furaha katika hilo.

Wahusika ni wote kuanzia mabingwa wa ligi ambao ni Yanga nao wana jukumu la kuongeza umakini kwenye usajili pamoja na maandalizi ya msimu ujao.

Singida Fountain Gate nao inawahusu bila kuwasahau Namungo mpaka Geita Gold. Maisha mapya ndani ya Championship kwa Mbeya City na Ruvu Shooting ni muhimu kufanya maandalizi mazuri.

Tunaona timu zinavuna kile ambacho walipanda kwa kuwa wanabainisha wana wataalamu ambao wanafuatilia aina ya wachezaji wanaohitaji.

Pia benchi la ufundi limekuwa likitoa ripoti ambayo inaamua kipi kifanyike kwa wachezaji wapya kusajiliwa na wengine kupewa mkono wa asante.

Kwa namna yoyote ile kuna vitu vya msingi ambavyo vinapaswa kufanyiwa kazi ikiwa itakuwa tofauti na mavuno nayo majibu yake yatakuwa mabaya.

Kama mchezaji atasajiliwa na hajafuatiliwa kwa muda mrefu hapo mavuno atakuwa amepata mchezaji na timu itaishia kumtangaza kuwa ni mchezaji mzuri na mwisho atabaki kuwa mtu wa kukaa benchi.

Ushindani ulivyo kwa sasa, kumsajili mchezaji kisha akawa anaanzia benchi mechi zote hiyo ni hasara kwa timu kwani mchezaji analindwa na mkataba kwa muda huo.

Vipengele ambavyo huwa vinaandikwa kuhusu uvunjanji wa mkataba na namna ya kuwaacha wachezaji ni ujanja wa akili kwa ili wapate faida.

Wakati mwingine hata viongozi nao wanatambua ubora wa wachezaji ambao wanawaleta kwa kuwa wapo kwenye mashindano na timu fulani wanalazimisha ushindi wa mezani lakini uwanjani ni hamna kitu.

Kikubwa umakini unahitajika na wachezaji ambao watapata nafasi kwenye timu mpya ni lazima wapambane kufanya kazi kwa ajili ya kutimiza majukumu yao.

Wachezaji wanapenda kupata timu mpya wanazopenda ili kupata changamoto mpya na changamoto mpya zinapenda kuwapata joto ya jiwe wachezaji.

Hakuna anayependa kushindwa basi wakati wa mavuno umakini hauwezi kuukwepa ni lazima waongeze.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: