Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulimwengu apewa masharti Singida FG

Thomas Ulimwengu SFG Ulimwengu apewa masharti Singida FG

Tue, 1 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Lile dili la nyota wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu tuliyowajulisha wiki iliyopita kuwa anajiandaa kutua Singida Fountain Gate, limetiki kwa mabosi wa klabu hiyo kumpa mkataba wa miaka miwili ukiwa na masharti ya kuongezewa kutegemeana na kiwango atakachoonyesha.

Nyota huyo aliyewahi kuwika TP Mazembe kisha kucheza JS Soaura na Al Hilal tayari amejiunga na kambi ya timu hiyo iliyopo mjini Singida kujiandaa na maandalizi ya msimu mpya na utambulisho utakaofanyika kesho kwenye tamasha la 'Singida Big Day', litakalofanyika mjini Singida.

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya timu hiyo ililiambia Mwanaspoti, kandarasi ya nyota huyo inaweza kuongezeka ingawa itategemeana na kiwango chake atakachokionyesha pindi atakapocheza.

"Ni mchezaji mzuri tunayeamini atatusaidia sana lakini mkataba huu umekuwa na masharti kidogo kwake kwa sababu ya kuhofia kiwango chake kwani hakucheza kwa muda mrefu," kilisema chanzo chetu.

Kwa upande wa kocha Hans Pluijm alisema usajili wao wote walioufanya msimu huu umezingatia mashindano mbalimbali wanayoshiriki hasa michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika.

"Msimu ujao utakuwa ni mgumu na wenye ushindani kwa sababu kila timu inaonekana wazi imejipanga vyema kuanzia maandalizi na usajili hivyo nasi kama sehemu hiyo lazima tuonyeshe ubora wetu."

Ulimwengu ambaye ni zao la Moro United pia aliwahi kucheza FK Sloboda Tuzla (Bosnia) na AFC Eskilstuna ya Sweden.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live