Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ulikuwa msimu mtamu kwao

Haaland X Saka Ulikuwa msimu mtamu kwao

Mon, 29 May 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu England imetaja majina ya mastaa saba kutoka klabu tano tofauti kwenye orodha ya watakaowania tuzo ya mchezaji bora wa msimu huu wa ligi hiyo. Tuzo za Mchezaji Bora wa msimu wa Ligi Kuu England zimeakuwa zikidhaminiwa na EA SPORTS tangu mwaka 2016 na zimekuwa zikitolewa kila mwaka tangu msimu wa 1994/95.

Kwa msimu huu wa 2022/23, Manchester City na Arsenal imetawala tuzo hiyo kwa kutoa mastaa wengi. Jina la Erling Haaland bila shaka limetajwa kwenye namba moja, kutokana na straika huyo wa Man City kufunga mabao 36 katika msimu wake wa kwanza wa ligi hiyo na kuvunja rekodi ya kufunga mara nyingi kuliko mchezaji yeyote kuwahi kufanya hivyo ndani ya msimu mmoja tangu ligi ilipoanza 1992.

Kwenye kinyang'anyiro hicho ataungana na staa mwenzake wa Man City, Kevin De Bruyne, ambaye amekuwa kinara kwa kuasisti, akipiga pasi za mabao kwa wachezaji wenzake mara 16.

Kwa upande wa Arsenal, msimu huu walikuwa kwenye msako wa kusaka taji lao la kwanza la Ligi Kuu England tangu mwaka 2004 na jambo hilo liliwafanya kucheza kwa ubora mkubwa uliowafanya wakali wake wawili, Martin Odegaard na Bukayo Saka kuingia kwenye kinyang'anyiro cha tuzo.

Odegaard alicheza kwa kiwango bora akiwa nahodha wa Arsenal, huku Saka naye akiwa kwenye ubora mkubwa akihusika kwenye mabao 24 yakiwa ya kufunga na kuasisti katika Ligi Kuu England.

Timu nyingine tatu zilizoingiza mastaa wake kwenye msako wa tuzo hizo ni Manchester United, atakayowakilishwa na Marcus Rashford, Tottenham Hotspur itakayobebwa na Harry Kane na Newcastle United - bendera yake itapeperushwa na beki wa kulia Kieran Trippier.

Kane amekuwa moto kwa kufunga mabao msimu huu na kwamba amezidiwa na Haaland tu, akiwa amefunga mara 28.

Mastaa Haaland, Odegaard na Saka watachuana pia kwa upande wa Kinda Bora wa Msimu, ambayo itashirikisha wachezaji wanane, huku kwa upande wa makocha watakaowania tuzo ni Mikel Arteta, Pep Guardiola, Eddie Howe, Marco Silva, Unai Emery na Roberto De Zerbi.

Wakati wakali hao wakisubiri tuzo ya kufunga msimu, hii hapa orodha ya waliobeba tuzo za ubora wa kila mwezi zilizotolewa kwenye Ligi Kuu England msimu huu, ambapo tamati yake itakuwa kesho Jumapili.

APRILI 2023

-Mchezaji Bora: Erling Haaland (Man City) Mechi: 4 Mabao: 6 Asisti: 2 -Kocha Bora: Unai Emery (Aston Villa) Mechi: 7 Ushindi: 5 Mabao: 11

MACHI 2023

-Mchezaji bora: Bukayo Saka (Arsenal) Mechi: 4 Mabao: 3 Asisti: 2 -Kocha bora: Mikel Arteta (Arsenal) Mechi: 4 Ushindi: 4 Mabao: 14

FEBRUARI 2023

-Mchezaji bora: Marcus Rashford (Man United) Mechi: 4 Mabao: 5 Kupiga mbili: 1 -Kocha bora: Erik ten Hag (Man United) Mechi: 4 Ushindi: 3 Mabao: 9

JANUARI 2023

-Mchezaji bora: Marcus Rashford (Man United) Mechi: 4 Mabao: 3 Ushindi Derby: 1 -Kocha bora: Mikel Arteta (Arsenal) Mechi: 3 Ushindi: 2 Mabao: 5

DESEMBA 2022

-Mchezaji bora: Martin Odegaard (Arsenal) Mechi: 4 Mabao: 3 Asisti: 3 -Kocha Bora: Mikel Arteta (Arsenal) Mechi: 4 Ushindi: 4 Mabao: 10

OKTOBA 2022

-Mchezaji bora: Miguel Almiron (Newcastle) Mechi: 6 Mabao: 6 -Kocha Bora: Eddie Howe (Newcastle) Mechi: 6 Ushindi: 5

SEPTEMBA 2022

-Mchezaji bora: Marcus Rashford (Man United) Mechi: 6 Mabao: 3 Asisti: 2 -Kocha bora: Erik ten Hag (Man United) Mechi: 6 Ushindi: 4

AGOSTI 2022

-Mchezaji bora: Erling Haaland (Man City) Mechi: 5 Mabao: 9 Hat-Trick: 2 -Kocha bora: Mikel Arteta (Arsenal) Mechi: 5 Ushindi: 5

Chanzo: Mwanaspoti