Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukweli mchungu kwa Fei Toto na Jezi ya Taifa Stars

Fei Hatrick Kiungo wa Azam FC, Feisal Salum "Fei Toto"

Tue, 17 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwa sasa kiungo wa klabu ya Azam fc Faisal salum (Feitoto) hana nafasi katika kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania chini ya kocha Adel Amrouche.

Watu wengi wamekuwa wana jaji kwa nini mchezaji ambaye kwenye Nbc Premier league anashikilia nafasi ya pili kwenye orodha ya wafungaji bora mpaka sasa akiwa nyuma ya Jean Beleke mwenye mabao (5), Fei toto akiwa na mabao (4) ndani ya ligi kuu Tanzania bara

Tukumbuke Feisal ni mchezaji anyecheza eneo la kiungo wa kati na pia anaweza kucheza kama kiungo wa kati mshambuliaji, Timu yetu ya Taifa kwa sasa inahitaji zaidi viungo wenye sifa ya kuwa na uwezo mkubwa wa kumiliki mpira, Uwezo mkubwa wa kukaba,Uwezo wa kukimbia umbali mrefu uwanjani endapo timu inapokuwa na mpira na pia timu inapokuwa nyuma ya mpira

Timu yetu ya taifa kwa sasa inahitaji sana kuwa na viungo kama Mudathiri, Mzamiru, Bajana, Himid Mao, Ambao wanasifa za kutengeneza uwiano mzuri katika eneo la kiungo dhidi ya Mpinzani, Timu kwasasa inahiatahi sana kupata wachezaji wenye uwezo wa kujitoa kitimu zaidi lakini sio ubora binafsi wa mchezaji ndani ya klabu yake

Chanzo: www.tanzaniaweb.live