Ukilisikiliza kauli ya Msemaji wa Coastal Union, Abbasi El Sabri utakubaliana na mimi kwamba bado kuna tatizo kubwa kwenye uongozi wa Costal Union kuhusu usajili wa Lameck Lawi kwenda Klabu ya Simba.
Awali viongozi wa Costal Union walishakubaliana na Simba, na Simba walishaweka pesa ya usajili kwenye account ya Costal Union, Lameck Lawi alishasaini mkataba wa miaka 3 na Simba na pia hata mechi ya mwisho ya ligi aliwaaga mashabiki wa Costal Union.
Isitoshe, hata Msemaji wa Costal Union alishawahi kunukuliwa akisema Costal wameshamalizana na Simba na wamemruhusu mchezaji kufanya makubaliano ya maslahi binafsi na Simba.
“Kwa Lameck Lawi ni kweli Simba wameleta ofay a beki wetu Lameck Lawi na hivi tunavyozungumza tumeacha wamalize maslahi binafsi lakini klabu tayari kuna mazungumzo ambayo yamekwisha afikiwa na kukubaliana, kilichobaki ni hatua ndogo tu ya kusaini mkataba lakini mazungumzo yetu yameshakwisha.
“Mchezaji wetu Lameck Lawi tayari mechi ya mwisho kabisa alishaaga mashabiki wetu na yuko tayari kwenda kupokea challenge mpya nje ya Coastal Union.
“Kwa Ley Matampi mazungumzo bado yanaendelea, sio tu kwa Tanzania bali hata nje ya Tanzania kuna mazungumzo yanaendelea, itategemea mazungumzo hayo yatamalizika vipi,” alisema Abbasi El Sabri.
Kinachotokea kuna baadhi ya viongozi waandamizi wa Costal Union hawakuhusishwa kwenye usajili wa Lawi hawajakubaliana na kitendo cha kuuzwa kwa mchezaji huyo, wanaitaji abaki kwa ajili ya kuichezea Costal kwenye michuano ya CAF, lakini kiuhalisia tayari wameshachelewa dili lilishakamilika.
“Timu zaidi ya moja zilionesha nia ikiwemo Simba, tulifanya nao mazungumzo na tuliwapa taratibu za kufuata kama kweli wanamtaka Lawi ,kwa bahati mbaya hawakufuata masharti tuliyowapa tukaamua ku-cancel na kuwaambia hatupo tayari kufanya biashara,” amesema alisema Abbasi El Sabri.
Inaelezwa kuwa, Coastal Union wameirudisha pesa ya Simba SC kwenye akaunti yao ya benki, nguvu wanapata kutoka kwa mfadhiri Binslum.
Aidha, Taarifa ya Lawi kutakiwa Ulaya ni kweli lakini sasa Coastal wamebadilisha mawazo wanataka kumtumia kwenye michuano ya kimataifa msimu ujao.
Simba yatoa tamko;
“Ndio tulichelewa kumaliza pesa, tulilipa nusu lakini mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yoye ya usajili.
"Tumemsajili Lameck Lawi kwa kufuata utaratibu. Wangesema kama ukichelewa kulipa mkataba unavunjika. Mpaka June tulikuwa tumemaliza kulipa pesa yote na nyaraka zote tunazo hata tukienda FIFA lakini Kilichotokea ni Coastal Union wakapata deal kutoka nje ndio maana wakabadili maamuzi.
"Tunafanya kazi kiweledi sana. Hoja yao ni dhaifu. Hoja yao pesa iwe imelipwa yote na kusema hawatambui mkataba. Mpira ni wa FIFA na hauishii hapa. Kiukweli hii imetusumbua na tutakabiliana nalo. Simba SC tumefuata taratibu zote za kumsajili Lameck Lawi,“ amesema Mjumbe wa Bodi ya Simba, Cresentius Magori.
Simba wanasema wamemalizana na Lawi, Coastal nao wanasema Lawi bado ni mchezaji wao na wana malengo nae kwa msimu ujao.
Nimeelewa kwanini Simba waliharakisha kumtangaza Lawi kabla hata hawajafanya photoshoot wakamtambulisha na bango la simba mnayama badala ya picha ya mchezaji. Inaonekana Coastal wanataka kufanya janjajanja.