Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukweli Kuhusu Bao la Geita Gold vs Simba

Video Archive
Thu, 2 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

NIMESHUHUDIA mchezo wa Simba dhidi ya Geita kwa dakika tisini, lakini pia nimetazama mara mbilimbili replay ya tukio lililopelekea watu wasijadili ubora wa mechi na kujikita zaidi kwa kumtazama mwamuzi Martin Saanya.

Ni goli halali, hakukuwa na mgusano uliompelekea Shomari Kapombe kuruka kiasi kile, Saanya pale amepepesa bila ubishi lakini katika tukio lile shujaa ni Kapombe, kwanini?.

Kapombe ameonyesha sifa ya mchezaji mkubwa na mwenye ukomavu, alifanikiwa kumdanganya mwamuzi kitu kilichopelekea Geita Gold wakataliwe goli lao.

Matukio ya aina ile huwa yanatokea sana katika mechi za mpira wa miguu na timu fulani kufaidika baada ya mwamuzi kuhadaiwa, leo haitakuwa mara ya kwanza wala si mara ya mwisho.

Tukiachana na hayo tuwapongeze Geita Gold, hii ni mechi ya tatu wanacheza na wakubwa katika uwanja wa ugenini na wanaonyesha mechi nzuri, kongole kwa vijana na hongera kwa mwalimu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live