Katika mechi tano mfululizo walizocheza Simba hawajaambulia clean sheet, (kucheza bila kuruhusu bao) zaidi ya kutunguliwa mabao sita.
Makosa yapo katika eneo la kiungo anapocheza Mzamiru Yassin, Fabricne Ngoma, beki anapocheza Henock Inonga, Che Malone, mlinda mlango Ally Salim, Ayoub Lakred.
Ni Ally Salim kosa lake kubwa ni katika kupangua mipira langoni mwake mingi inaishia katika eneo alilopo inakutana na wapinzani.
Ilikuwa hivyo dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa. Ongeza kosa lingine Timu hiyo chini ya Kocha Mkuu, Roberto Oliveira katika hatua ya robo fainali ya African Football League iliruhusu mabao matatu dhidi ya Al Ahly.
Mchezo wa kwanza Uwanja wa Mkapa ubao ulisoma Simba 2-2 Al Ahly na ule wa pili ilikuwa Al Ahly 1-1 Simba na wakaondolewa kwa kanuni ya mabao ya ugenini ikiwa ni faida kwa Al Ahly.