Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukuta, kiungo Taifa Stars usipime!

Msuva Stars Banda Job Novatus Ukuta, kiungo Taifa Stars usipime!

Thu, 16 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

kikosi cha timu ya taifa, Taifa Stars kinatarajiwa kupaa leo kwenda Morocco kwa mchezo wa kwanza wa Kundi E wa kuwania kufuzu ushiriki wa fainali za Kombe la Dunia 2026, huku benchi la ufundi la timu hiyo likitambia ukuta na kiungo kilichobeba tumaini kwenye mchezo huo dhidi ya Niger.

Mchezo huo wa Stars na Niger unapigwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Marrakech, mjini Marrakech, Morocco ambao wenyeji Niger wanautumia kama uwanja wa nyumbani kabla ya Stars kurejea nchini kuikaribisha Morocco iliyopo kundi moja mapema wiki ijayo.

Stars ikijiandaa kwa mechi hizo mbili za awali, Mwanaspoti linachambua kikosi hicho ambapo jana tulianza na eneo la makipa ambako kuna vita nzito kwa makipa watano waliochaguliwa kwa sasa na leo tunaendelea kuangalia eneo la ulinzi na kiungo kunavyoweza kuibeba timu hiyo kwenye kundi hilo.

VITA ILIVYO

Kama ilivyo kwenye eneo la kipa, katika kikosi cha Stars kambini kabla ya leo kuanza safari ya kwenda Morocco, kuna vita ya namba kwenye ukuta na kiungo cha timu hiyo na unaweza kusema patachimbika.

Kocha wa Stars, Adel Amrouche amewajumuisha mabeki 12 na viungo 9 kwenye kikosi hicho, lakini ni wazi kwamba wachezaji wanane pekee ndio wanatakiwa kupata nafasi ndani ya mchezo mmoja.

Kumbukumbu zinaonyesha kocha Adel anatumia mfumo wa 3-5-2 ndio chimbuko la kocha huyo kuwa na desturi za kuita mabeki wengi na viungo kwenye kikosi chake

UKUTA YANGA

Hakuna shaka kwamba katika uamuzi wa Amrouche kuanza na mabeki watatu ataendelea kuwaamini mabeki watatu Dickson Job, Bakari Mwamnyeto na Ibrahim Hamad ‘Bacca’ ambao wote wanacheza pamoja kwa nyakati tofauti pale klabuni kwao Yanga.

Mabeki hao tayari wameshatengeneza kemia nzuri baina yao ambao wataendelea kuwa pamoja baada ya kuonyesha utulivu mkubwa kwenye mechi zilizopita.

Kwa ubora waliouonyesha mabeki wawili wa pembeni ambao pia wanacheza kama mawinga Haji Mnoga na Novatus Dismas wataendeleza ubora wao katika kuiunganisha timu wakati wa kushambulia wakibadilika kuwa mawinga, pia kushuka kuongeza idadi ya mabeki kuwa watano wakati timu inapopoteza mpira.

Katika kikosi hicho, kocha amewaita Dickson Job, Bakar Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Lusajo Mwaikenda, Nickson Kibabage, Haji Mnoga, Abdi Banda, Novatus Dismas, Edward Manyama, Abdulmalik Zakaria, Omary Mvungi na Edwin Balua.

HAPO KATI VIUNGO WATATU

Licha ya Novatus na Mnoga kuwa kama sehemu ya viungo kwa mfumo huo pia viungo wanne ambao watatu kati ya hao wanaweza kuingia ndani ya kikosi hicho ni Mudathir Yahya, Himid Mao, Sospeter Bajana na Feisal Salum ‘Fei Toto’.

Viungo hao Amrouche atachagua wawili kuwa kama wakabaji kati ya Bajana, Mudathir na Himid kulingana na nidhamu yao ambayo wataionyesha.

Juu yao kunaweza kuwa na kiungo mmoja mchezeshaji atakayeunganisha timu hiyo kutoka chini na washambuliaji wa juu na kwa kiwango cha sasa cha Fei Toto anaweza kuwa mtu muafaka kuanza eneo hilo.

Mchango mwingine unaompa nafasi kubwa Fei toto ni jinsi ambavyo amekuwa na nguvu ya kuongeza kasi wakati wa kushambulia na ubora wa kufungat.

Safu nzima inaundwa na Ibrahim Joshua, Mzamiru Yassin, Sospeter Bajana, Feisal Salum, Mudathir Yahya, Morice Abraham, Himid Mao na Ladaki Chasambi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live