Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukizubaa umepotea Nusu Fainali Kagame Cup leo

Screenshot 20210811 075758 Instagram Patashika za Michuano ya Kombe la Kagame

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Matajiri wa Jiji la Dar es Salaa,Azam FC leo itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Big Bullets ya Malawi katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Kagame.

Mchezo huo utakaopigwa majira ya saa 1:00 usiku, katika Uwanja wa Azam Complex unatarajiwa kuwa wa ushindani kwa timu zote mbili kupambania nafasi ya kutinga hatua ya fainali.

Azam watahitajika kufanya kazi ya ziada kwa dakika zote 90,kwa kuwa Big Bulllets imekuja kikamilifu na wachezaji wake wote wa kikosi cha kwanza tofauti na Azam ambao vijana wao wengi sio wale wenye uzoefu .

Mshindi wa mchezo wa leo kati ya Azam na Big Bullets, atakutana fainali na Express ambayo ilishinda nusu fainali ya kwanza Uwanja wa Azam Complex mbele ya KMKM kwa mabao 2-1,Agosti 10.

Kwa mujibu wa Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit "Zaka zakazi" amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa leo na wanahitaji ushindi ili kutinga hatua ya fainali,lakini kubwa ni kutengeneza historia kwa vijana wenyewe walioamua kuwatumia kwenye michuano hiyo.

Mara zote ambazo Michuano ya kombe la Kagame imechezwa hapa nchini,Klabu ya Azam haijawahi kushindwa kufika hatua ya fainali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live