Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukiweza kumfunga yanga 4, yeye anakufunga 6 - Mexime

Mexime Yanga Kocha Mecky Maxime

Sat, 18 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Ihefu FC, Mecky Mexime amesema ili kujisifu una timu bora ni lazima ucheze na timu yenye bora kama ambavyo yeye na vijana wake wapo tayari kucheza dhidi ya Yanga kesho kwenye mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la Shirikisho CRDB.

Mexime ametoa kauli hiyo leo wakati akizungumzia maandalizi ya mchezo huo ambapo amesema anafahamu ubora walionao Yanga lakini wachezaji wake hawapaswi kuingia kinyonge katika mchezo huo.

“Watu wengi wanawapa sana nafasi Yanga kutokana na washakuwa mabingwa na kweli wana timu bora lakini na sisi tumeitengeneza timu yetu , sasa ukitaka kuifunga timu bora lazima na wewe timu yako iwe bora kwahiyo na sisi tuna timu bora,” amesema Mexime na kuongeza

“Yanga yeye anajiamini ana watu wanaweza kuimaliza mechi ,haangalii utamfunga ngapi huwa anaangalia atakufunga ngapi kama unaweza kumfunga nne yeye atakufunga sita, kwahiyo inabd tuangalie tutacheza vipi karata zetu, “amesema kocha huyo.

Mchezo huo wa Nusu Fainali ya pili utapigwa Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Arusha majira ya 9:30 alasiri.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live