Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukiwa upande wa lile Goli 1, Bango la Yanga utaona ni ushamba

Yanga Bango Ukiwa upande wa lile Goli 1, Bango la Yanga utaona ni ushamba

Tue, 14 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Hiki wanachokifanya Yanga SC sio kumkera tu mtani bali ni kutoa 'Mileage kwa wadhamini wao kuonekana zaidi na watu, wanawatangaza zaidi, umefikiria ni watu wangapi wameliona hili bango? Ni watu wangapi wameshare hili bango ? Kiuchumi ina tija kubwa sana.

Hii ndio maana ya utani wa jadi, ukimuotea mwenzako mpige kweli na ujisifie kweli ili wakati wote aone unyonge ili naye ajipange vyema zaidi.

Huu sio ushamba bali ni utani na hamasa kuelekea Derby ijayo.Sidhani kama kuna mtu anaweza kuwa mnyonge kwenye mchezo ujao.

Vita hii sasa tuihamishie kimataifa, huko kila mmoja amtambie mwenzake kwa aina yake anayojua ili apambane kwa hali na mali.

Hapa kuna mdhamini gani atakataa kuja kuidhamini Yanga? Kwa namna ambavyo wanawafanya wadhamini wao waonekane?

Hongereni Wananchi.

Yanga bwana Usikute wameomba dakika zote 90 za mchezo ule ziwekwe Youtube, au usikute wamechapisha na vipeperushi vidogo vidogo Hawashindwi hawa kama waliweza kunywa supu kwenye mvua na mafuriko washindwe hili

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: