Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukiwa na hii timu, makombe yote unabeba

Timu Pic Data Ukiwa na hii timu, makombe yote unabeba

Sun, 11 Apr 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

LONDON, ENGLAND

MSIMU wa soka wa 2020/21 unakaribia ukingoni na jambo hilo litashuhudia pia mastaa kibao mikataba yao ikifika tamati kwenye timu wanazocheza na watakuwa huru kuondoka kwenda kuanza maisha kwingineko.

Kitu kinachovutia ni kwamba kwenye orodha ya mastaa ambao mikataba yao inatarajia kufika tamati wapo wakali kabisa ambao kama ikitokea umewanasa wote na kutengeneza timu moja, basi utabeba kila taji utakaloshindania.

Cheki timu yenyewe hii hapa - nani atatoka kwenye kikosi kama hicho. Wapinzani watapigwa nyingi uwanjani.

Kipa: Gianluigi Donnarumma (AC Milan)

Utashangaa kwa umahiri wake wote Donnarumma ndo kwanza ana umri wa miaka 22 na kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi anaweza kuachana na AC Milan kwa sababu mkataba wake kwenye timu hiyo utakuwa umefikia tamati. Chelsea imehusishwa mara kadhaa kuhitaji huduma yake ambayo itapatikana bure kabisa.

Related WAACHE WAUANE, Huko Ulaya unapigwa muda woteBeki wa kati: Jerome Boateng (Bayern Munich)

Imethibitishwa kwamba Boateng ataachana na Bayern mwishoni mwa msimu huu kutokana na mkataba wake kumalizika, hivyo timu yoyote itakayohitaji saini yake itakuwa na nafasi ya kumchukua bure kabisa. Hakuna ubishi kiwango chake cha msimu wa 2019/20 kitampa dili safi kabisa kujiunga na klabu kubwa.

Beki wa kati: Sergio Ramos (Real Madrid)

Hakuna ubishi, Ramos ni mmoja wa mabeki bora kabisa wa kati na bila ya shaka timu itakayofanikiwa kunasa saini yake itakuwa imepiga bao muhimu. Mkataba wa beki huyo utafika tamati mwishoni mwa msimu huu, hivyo atakuwa huru kuachana na Los Blancos na kwenda anakotaka. Huduma yake inasakwa na miamba kibao Ulaya.

Beki wa kati: David Alaba (Bayern Munich)

Baada ya kutamba na kikosi cha Bayern Munich kwa miaka kadhaa, Alaba sasa ni rasmi kwamba ataachana na miamba hiyo ya Ujerumani mwishoni mwa msimu huu wakati mkataba wake utakapofika tamati. Real Madrid imekuwa ukihusishwa na mchezaji huyo, ambaye itapata huduma yake bila ya kutoa mkwanja wowote dirisha lijalo.

Wing-Back wa kulia: Lucas Vazquez (Real Madrid)

Vazquez si jina maarufu sana kwenye kikosi hiki moto kabisa, lakini klabu zitakazofanikiwa kunasa saini yake zitapata huduma bora bora kabisa kutoka kwa mshindi huyo mara tatu wa Ligi ya Mabingwa Ulaya na amecheza mechi zaidi ya 200 akiwa na kikosi cha Los Blancos. Tottenham wamekuwa wakihusishwa na mpango wa kunasa huduma yake.

Wing-Back wa kushoto: Memphis Depay (Lyon)

Amekuwa kwenye kiwango bora kabisa tangu alipoachana na Manchester United na Depay sasa jina lake linahusishwa na timu kubwa Ulaya ikiwamo Barcelona. Staa huyo wa Kidachi aligoma kuongeza mkataba mpya kwenye kikosi cha Lyon, hivyo atakuwa mchezaji huru mwishoni mwa msimu huu na timu zitanasa saini yake bure kabisa.

Kiungo wa kati: Luka Modric (Real Madrid)

Huu ni kama utani, lakini habari ndo hiyo kwamba Modric atakuwa huru kujiunga na timu yoyote bure kabisa kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi kutokana na mkataba wake kufika ukomo mwishoni mwa msimu huu. Kuna timu kadhaa zinahitaji saini ya kiungo huyo fundi wa mpira na hakika zikimnasa zimefanikiwa.

Kiungo wa kati: Ge-orginio Wijnaldum (Liverpool)

Hapewi thamani yake anayostahili kwenye kikosi cha Liverpool, lakini hakuna ubishi Wijnaldum ndiye injini ya miamba hiyo ya Anfield. Lakini, mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu huu na hapo atakuwa mchezaji huru kujiunga na timu anayohitaji kwenda kwa sababu atapatikana bure huku Barcelona wakihitaji huduma yake.

Kiungo wa kati: Hakan Calhanoglu (AC Milan)

Ni mmoja wa wachezaji wenye thamani kubwa kwenye kikosi hiki na hakika Calhanoglu amekuwa akizivutia timu nyingi za Ligi Kuu England zikihitaji saini yake kutokana na kile ambacho amekuwa akifanya AC Milan. Arsenal na Chelsea zimekuwa zikifukuzia saini ya mchezaji huyo ambaye mkataba wake utafika tamati mwishoni mwa msimu.

Mshambuliaji: Lionel Messi (Barcelona)

Ndio hivyo. Supastaa, Lionel Messi ni mmoja wa wachezaji watakaopatikana bure kabisa kwenye dirisha lijalo la uhamisho wa majira ya kiangazi kutokana na mkataba wake kufika tamati huko Barcelona. Mabosi wa timu hiyo, akiwamo rais Joan Laporta wanahaha kuhakikisha anasaini dili jipya ili kubaki Nou Camp, la Messi atakuwa huru.

Mshambuliaji: Sergio Aguero (Man City)

Ni ngumu kueleza, lakini ndiyo hivyo imeshathibitishwa kwamba straika Sergio Aguero ataachana na Manchester City mwishoni mwa msimu huu wakati mkataba wake utakapofika tamati kwenye timu hiyo aliyochezea kwa miaka 10. Bado haifahamiki staa huyo atakwenda wapi, lakini Chelsea inatajwa kuwa moja ya timu zinazomfukuzia supastaa huyu mbabe.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz