Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukiwa na buku tano tu unaishuhudia derby

Kariakoo Dabi Mashabiki Ukiwa na buku tano tu unaishuhudia derby

Sun, 14 Apr 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Mashabiki wa Simba na Yanga wameanza kuhesabu siku kabla ya kupigwa kwa Kariakoo Derby, huku viingilio vya pambano hilo la 112 katika Ligi ya Bara tangu mwaka 1965 vikiwekwa hadharani na mashabiki hao wakiwa na buku tano tu, wanaruhusiwa kuingia Kwa Mkapa kushuhudia timu hizo zikiumana.

Simba na Yanga zitavaana Jumamosi ijayo (Aprili 20) kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam huku zikiwa na kumbukumbu ya matokeo ya mechi iliyopita ya kwanza kwa msimu huu iliyopigwa Novemba 5 mwaka jana na Mnyama alinyooshwa kwa mabao 5-1 na kumtimua Kocha Roberto Oliveira 'Robertinho'.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa na Bodi ya Ligi (TPLB), kiingilio cha chini kuziona Simba na Yanga kwa Mkapa ni Sh5,000 tu.

Viingilio hivyo vilivyotangazwa kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya bodi hiyo inayosimamia Ligi Kuu Bara, cha juu kabisa ni Sh50,000 kwa VIP A, wakati VIP B ni Sh30,000 na VIP C ni Sh20,000, ilihali kwa upande wa viti vya rangi ya machungwa 'Orange' ni Sh10,000 tu.

Wadau wamekuwa na maoni tofauti katika uwanja wa maoni kutokana na taarifa hiyo ya bei za viingilio katika mchezo huo ambao una nafasi ya kuamua vita ya kuwania ubingwa wa Ligi Kuu kati ya vigogo hao.

Fodio349; "Na sisi Simba matokeo tushayajua hatuji uwanjani."

Ckazier; "Kama kuna uwezekano pia tunaomba tiketi ziwe na namba za kiti mtu atakachokalia."

Ngumbetwaib; "Ninyi mnatangaza viingilio kama nani mbona mnakuwa wa ovyo hivyo acheni tamaaa mpoje ninyi."

Ammylove_tz_4; "Kwani nyinyi hii mechi inawahusu nini hadi mpange viingilio?."

Mara ya mwisho watani hao wa jadi walipokutana katika ligi, Simba ilikumbana na kipigo cha mabao 5-1 hivyo mchezo huu utakuwa wa kisasi, heshima na vita ya kupigania ubingwa wa ligi ambayo Yanga inaongoza ikiwa na pointi 52, Azam inashika nafasi ya pili (47) huku Mnyama ikiwa na pointi 46.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: