Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukiwa na Aziz Ki, Guede atafunga sana - Shabiki Simba

Guede Aziz Ki Ukiwa na Aziz Ki, Guede atafunga sana - Shabiki Simba

Tue, 27 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shabiki maarufu wa Klabu ya Simba, anayefahamika kwa jina la Mchome amesema kuwa uwepo wa Aziz KI kwenye eneo la kiungo wa ushambuliaji wa Yanga, mshambuliaji mpya wa timu hiyo, Joseph Guede atafunga sana tofauti na watu ambavyo walikuwa wakimdhania.

Mchome amesema hayo baada ya Joseph Guede raia wa Ivory Coast kuanza kuonesha umwamba wake kwenye kikosi cha Yanga ambapo mpaka sasa amefunga mabao matatu kwenye michezo miwili ya mwisho licha ya kuanza vibaya wakati akijiunga na Wananchi.

Guende alifunga mabao mawili kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho wakati wa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Polisi Tanzania huku mabao yake yote akipewa assist na Augustine Okrah.

Aidha, Guede amefunga bao muhimu kwenye mchezo wa raundi ya tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika wakati timu yake ikiichabanga CR Belouizdad bao 4-0 na kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiy.

“Aziz Ki akiwepo uwanjani anatuliza presha ya timu, ukiwa na mchezaji kama huyo ni muda wowote anakupa assist au anakufungia, hata mabeki, mawinga na viungo wanakuwa na uhuru wa kufanya lolote.

“Ukiwa na Aziz Ki, Joseph Guede anakuwa huru kwa sababu mabeki wanamtazama zaidi Aziz, akishika mpira wanamkodolea macho yeye, halafu wanamwacha huru Guede, akipewa mpira Guede kazi yake kufunga tu. Ndiyo maana nilisema, Guede kufunga ni suala la muda tu,” amesema Mchome.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: