Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukitaka kuimaliza Yanga, mtoe kikosini huyu jamaa

Khalid Auchoooooooo Ukitaka kuimaliza Yanga, mtoe kikosini huyu jamaa

Mon, 26 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kuhusu mjukuu wa Milton Obote, Khalid Aucho nilikuwa nimefunga mjadala wa lakini acha nizungumze kitu.

Tutamsema sana kuhusu rafu sijui aggressiveness, yes bahati mbaya anacheza eneo linalohtaji yeye kuwa hivyo.

Aucho ukimtazama kwa jicho la mabao na assist basi utataka kumuondoa katika list ya viungo bora, na ni ngumu wachezaji bora kama hawa kupata tuzo ya kiungo bora kwenye ulimwengu huu wa numbers.

Lakini muangalie Aucho bila mpira au tiu yake imiwa haina mpira, ni mtu anayefanya mambo mengi sana ya kuiweka salama tmu yake na nyavu za Diarra.

✅Aucho anawania mipira ya hamsini kwa hamsini ✅Aucho pasi zake za kuvunja kiungo cha mpinzani ni sumu kali na silaha kubwa kwa Yanga ✅Aucho anajiweka rehani pale inapobidi ili kuiokoa timu yake ✅Atarusha konga, pepsi msingi timu yake iwe salama ✅Aucho anarudisha umiliki kwa timu yake wakiwa wanausaka mpira.

Aucho ni ndiye ameshika ufunguo wa Yanga, yeye ndiye anaamua timu ishambulie wakati gani na timu izuie wakati gani.

Mabeki wa Yanga wakipata mpira wanajua mtu wa kwanza kumtazama ni Aucho na yeye akishapata mpira tu utaona viungo wote wa Yanga na washambuliaji wao wanaanza safari kuelekea kwenye lango la mpinzani wakijua hii ni signatory kwaba tunakwenda kushambulia aidha kupitia pembeni au katikati.

Usahihi wa pasi za Aucho unawarahisishia kazi kina Pacome, Aziz Ki na Maxi Nzengeli wanapoelekea kutimiza mpango wao wa kusaka bao langoni kwa mpinzani.

Tusimuone Mudathir anafunga yale mabao, ni kwa sababu ana uhakika kwamba anapoondoka kwenda kuongezeka mbele kama mshambuliaji wa ziada kwenye boksi la mpinzani, nyuma amemwacha Aucho mwenye tank lake na ana uhakika wakipoteza mpira, kuna ulinzi madhubuti kabla ya kufikiwa mabeki wao.

Hiki ni kiungo ambacho kwa bahati mbaya tumekuwa tukisema pale anapocheza rafu tu badala ya kuweka wazi ubora wake. Siku akifanya vyema huwezi ona akiimbwa anavyo stahili, tunasubiri rafu ndo tuimbe hapo hapo.

Aucho ni kiungo ambaye hazungumzwi ipasavyo, thamani yake kwa timu yake na ligi yetu ni kubwa sana. Yeye ameacha miguu yake iongee, lakin Uganda wanajua thamani yake, jina lake katika mitaa yake na taifa lake ni kubwa sana.

Ni mara chache sana kumkuta Aucho akawa hayuko mchezoni, timu inapokuwa kwenye presha yeye ndiye anaituliza. Tazama mechi muhimu ambazo Aucho amekosekana pale katikati, Yanga wametaabika sana.

Huyu tuendelee kumsema tu kwa rafu lakini he is one among the best DM we ever Had in our League. Huyu ndiye Khalid Aucho, Daktari wa Mpira, The Tank.... Top Top Top Player.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live