Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukipigwa tano, tulia jipange

Yanga Bango Ukipigwa tano, tulia jipange

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kwenye mchezo wa mpira wa miguu, kufungwa mabao matano au zaidi katika mchezo mmoja ni jambo linaloumiza sana.

Sio rahisi kwa shabiki, kiongozi, kocha, mchezaji au mtu yeyote aliyepo kwenye timu iliyofungwa mabao matano katika mchezo mmoja akawa na furaha labda Jean Baleke ndio anaweza kufanya hivyo.

Tena hasa inapotokea idadi hiyo kubwa ya mabao, timu imefungwa katika mechi ya watani wa jadi kama ilivyotokea kwa Simba iliyofungwa mabao 5-1 na Yanga, siku ya Jumapili, Novemba 5.

Ndio ni watu wachache kama Baleke ambao wanaweza kuwa na nyuso za furaha pale timu yao inapofungwa mabao mengi kama matano, si ulimuona siku ile baada ya mechi ya Yanga yeye akawa anacheka tu kwa furaha na wenzake utadhani timu yake ndio ilishinda kumbe walipasuka nyingi.

Sasa kunapoibuka matokeo kama hayo kama tunavyozijua timu zetu, huwa zile zinazofungwa zinajitahidi sana kufanya mambo ya kusahaulisha machungu ya kuchapika na zile zinazoshinda huhakikisha zinakumbushia kila mara kibano kilichotoa kwa mtani.

Lakini kwa timu inayofungwa tena goli nyingi, mara kwa mara njia bora ya kusahau machungu huwa ni timu kuonyesha kiwango bora katika mechi zinazofuata, kupata ushindi na pia kutwaa mataji hapo kidogo mashabiki watapata cha kutambia upande ule uliowafunga nyingi.

Ni vigumu kwa shabiki kumaliza machungu ya kufungwa tano na mtani kwa timu kusifiwa tu pasipo kufanya vyema uwanjani hasa katika nyakati ambazo timu yake inaonyesha ina uwezekano duni wa kutwaa mataji au kulipa kisasi cha kichapo kwa mtani.

Kwa kilichoikuta Simba hivi karibuni, mashabiki wanataka kusikia kauli ambazo pengine zitawafanya waone viongozi wao waliguswa na kipigo walichokipata na wanaandaa mikakati mizuri ya kuirudisha timu kwenye mstari.

Yatolewe matamko machache ambayo yatarudisha imani na tumaini la mashabiki kwa timu badala ya mengi ambayo yanaishia kuwachanganya tu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live