Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukimshabikia Ronaldo huwezi kumjua Messi

Mabppe Messi Ronaldo Ds Ukimshabikia Ronaldo huwezi kumjua Messi

Thu, 14 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mshambuliaji wa Klabu ya PSG, Kylian Mbappe amesema kuwa amekuwa shabiki wa Cristiano Ronaldo tangu akiwa mdogo hivyo kutokana na mapenzi yake kwa staa huyo, hakuwahi kuujua ubora wa Lionel Messi.

Mbappe (24) ambaye ni mchezaji wa Timu ya Taifa ya Ufaransa amekuwa akionyesha mahaba yake kwa Ronaldo wazi wazi lakini hata alipopata wasaa wa kucheza na Messi pale PSG misimu miwili iliyopita, hakuonyesha kumfagilia kabisa jamaa.

Hii ni kauli ya Mbappe; "Nampenda Cristiano Ronaldo, tangu nikiwa mtoto nimekuwa shabiki wake mkubwa.

"Lakini nimeanza kujifunza sasa kwa sababu unapokuwa shabiki mkubwa wa Ronaldo huwezi kuona jinsi gani Lionel Messi alivyokuwa mzuri kwa sababu unampenda Ronaldo lakini nimekuwa sasa na ninawapenda wote wawili sasa," amesema Kylian Mbappe.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: