Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukicheza dhidi ya Messi utatamani umuue - Ramos

Ramos Messi 729 16 9 Ukicheza dhidi ya Messi utatamani umuue - Ramos

Tue, 27 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bekio wa zamani wa real Madrid na PSG, Sergio Ramos García amesema kuwa hakuna kazi ambayo mabeki wamekuwa wakiipata kama kumbaka aliyekuwa mshambuliaji wa Barcelona, Lionel Messi.

Ramos amesema hayo baada ya wawili kucheza timu moja ya PSG na baadae kila mmoja kuhama na kwenda timu nyingine ambapo Messi yupo Inter Miami ya Marekani, wakati Ramos akirejea kwenye klabu yake ya zamani ya Sevilla.

"Ukicheza dhidi ya Messi utatamani umuue, ila ukicheza naye kwenye timu moja utatamani umuue kila anayejaribu kumgusa. Yeye ni mshambuliaji hatari zaidi niliyewahi kukabiliana naye, na mabeki wote kutoka La Liga watakuambia hili".

"Tulipoanza kucheza kwenye timu moja, tukiwa uwanjani nilikuwa nikijisemea 'Nacheza kwa amani sasa, Messi yupo upande wangu sio kwa wapinzani'.

"Walinzi wa sasa hawawezi kujua maumivu tuliyopitia wakati tunakabiliana naye, yeye ni mchezaji bora zaidi kwenye historia ya mpira wa miguu na kila mtu anatambua hilo," Sergio Ramos.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live