Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukata wa Fedha waitikisa Gor Mahia, Wachezaji tisa tu wafanya mazoezi

Gormahia FC UKATA Kikosi cha Gor Mahia

Sun, 18 Sep 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida, wachezaji tisa pekee wamekuwa wakijitokeza kwenye mazoezi ya kujiandaa na msimu ujao wa mashindano ya kikosi cha Gor Mahia.

Sababu inayoelezwa ya wachezaji kutojitokeza kwenye mazoezi ni mgomo baridi wa kushinikiza malipo ya mishahara na marupurupu mengine ambayo waliahidiwa kwa zaidi miezi miwili iliyopita.

Wakati hayo yakitokea, msisitizo mkubwa wa viongozi wa Gor Mahia ni kuwa kocha amepanga kuyafanyia kazi makosa kwenye kila eneo uwanjani, kwa sasa ameanza eneo la ulinzi ndiyo sababu wachezaji wanaonekana wachache, Jolawi Obondo alisema Meneja wa Gor Mahia ambao ni mabingwa mara 19 wa Ligi Kuu nchini Kenya FKFPL.

“Kocha (Johnathan McKinstry) amekuwa akifanya hivyo ili kuinoa kila safu moja baada ya nyingine, siyo jambo geni”.

Hata hivyo inaonekana ni zaidi ya hapo kwani mchezaji mmoja ambaye hakutaka jina lake kuwekwa hadharani kwa hofu ya kufanyiwa vitimbwi alisema viongozi wamekuwa wakiongea uongo kwenye vyombo vya habari lakini ukweli ni kuwa wachezaji wako kwenye mgomo wa kutaka kulipwa stahiki zao.

Mchezaji huyo alienda mbali na kusema hata pale ambapo wakilipwa wamekuwa wakipewa nusu ya makubaliano ya kimkataba.

Wakati hayo yakiendelea, wadau wa soka wameendelea kujiuliza inakuwaje Gor Mahia washindwe kuwalipa wachezaji mishahara wakiwa kwenye moja ya mkataba imara na kampuni moja ya ubashiri nchini humo.

Itakumbukwa mwezi Julai 2022 Gor Mahia walisaini mkataba wa miaka mitatu wenye thamani ya milioni Ksh 76.5 (Tsh 1,480,481,312) na kampuni hiyo lakini muda mfupi baadaye malalamiko kama hayo yanatokea.

Mmoja ya mdau wa soka nchini humo ameeleza kuwa kampuni ya kubashiri iliyoingia mkataba na K’Ogalo haina fedha kwa sasa hivyo imekuwa ikikiuka masuala mbalimbali ya kimkataba.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live