Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ukata, Uganda wajiondoa Michuano ya CHAN 2023

Uganda Team Kikosi cha Uganda

Wed, 14 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Taifa ya Uganda ‘The Cranes’ imejiondoa kushiriki Fainali za Mataifa Bingwa Barani Afrika ‘CHAN’ zitakazorindima mapema mwaka 2023 nchini Algeria.

Uganda ilipata tiketi ya kushiriki Fainali hizo kwa kuifunga Tanzania ‘Taifa Stars’ mabao 4-0, baada ya michezo ya nyumbani ya ugenini.

Rais wa Shirikisho la soka Nchini Uganda ‘FUFA’ Moses Magogo amesema sababu kubwa ya kujitoa katika Fainali hizo ni kutokana na ukata wa fedha unaowakabili kwa sasa.

Tayari Uganda imeshatuma barua CAF ya kujiondoa kwenye Michuano hiyo, ambayo imepangwa kuanza kuunguruma Januari 13 hadi Februari 04 mwaka 2023.

Uganda imepangwa Kundi B lenye timu za DR Congo Ivory Coast na Senegal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live