Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujio wa Yao ni somo kama ilivyokuwa kwa Diarra

Yao Yao Kmc Mlinzi wa kulia wa Yanga, Yao Kouassi

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ujio wa Diarra ulikuja kutuonyesha Utofauti na Ubora wa makipa wetu tuliokuwa tunaamini ni bora kwa muda mrefu,

Pia hata kwa Yao amekuja kutuonyesha maana halisi ya Mlinzi bora wa pembeni anatakiwa afanye awapo Uwanjani,

NANI KASEMA KIBWANA SHOMARI AMESHUKA KIWANGO ?

Yawezekana ndilo neno linaloongoza kukaa midomoni mwa watu pindi wasipomuona kiwanjani ama akiwa kwenye mbao ndefu,

Jua kwamba Usajili wa Yao ndani ya Yanga ulikuwa na lengo la kupata mlinzi mzoefu na mwenye Ubora katika eneo la upande wa kulia wa Young Africans katika Michezo ya kimataifa,

Ubora wa Yao kouassi umetengeneza tabaka kubwa sana Kibwana Shomari, hapa nazungumzia Ubora wake awapo Uwanja katika maeneo 3 kwa maana kujilinda, kuchezesha na kushambulia,

Yao Kouassi hajaleta utofauti na kibwana Shomari tu bali ameleta tupate darasa kwa walinzi wote wa pembeni zaidi ni wale wanaocheza Upande wa upande wa kulia,

Kwasasa ndani ya NBC ni vigumu sana kumlinganisha Mlinzi Yao na walinzi wengine, na hii ni kutokana Ubora wake mkubwa,

Yao ameleta Utofauti mkubwa sana na Tuliokuwa tuna amini ni bora kwa Upande wa kulia na ndio maana tumekuwa tukiona On and Off zao kwasasa kupitia Ubora na matukio ya Yao awapo Uwanjani,

Sio kwamba Yao bora sana ila ametuonyesha Ubora wake kwa zaidi ya 70% katika eneo analokuwepo yaani

Kujilinda

Kuchezesha/kutengeneza

Kushambulia

Utofauti na Wazawa Wamekuwa wakikupa kimoja kati ya 3 kwa Ubora iwe kujilinda ama kushambulia,

Yao ndio darasa halisi la mlinzi bora wa kulia anavyotakiwa kucheza na matukio yote Uwanjani.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: