Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujerumani wapigwa marufuku kununua jezi nambari 44 - kunani?

Ujerumani Wapigwa Marufuku Kununua Jezi Nambari 44   Kunani Ujerumani wapigwa marufuku kununua jezi nambari 44 - kunani?

Tue, 2 Apr 2024 Chanzo: Bbc

Kampuni ya Adidas imewapiga marufuku mashabiki wa soka kununua jezi ya mpira wa miguu ya Ujerumani yenye nambari 44, baada ya vyombo vya habari kusema inafanana na nembo iliyotumiwa na vitengo vya SS vya Vita vya Pili vya Dunia.

"Tutazuia ubinafsishaji wa jezi, hiyo" msemaji wa Adidas alisema.Vitengo vya SS ndivyo vilivyohusika zaidi na uhalifu dhidi ya ubinadamu uliofanywa na Wanazi.

Seti hiyo mpya jezi mpya iliyotolewa pia imezua utata na uchaguzi wake wa rangi ya waridi kwa ajili ya rangi za ugenini.

Suala la nembo lilitolewa kwa mara ya kwanza na mwanahistoria Michael König, ambaye alisema muundo wa jezi hiyo "unatia shaka sana".

Nembo ya SS iliundwa mnamo 1929 kwa matumizi ya vitengo vya Nazi. Washiriki wa SS walishirikisha maajenti wa Gestapo hadi walinzi wa kambi ya mateso.

Majukumu ya SS yalikuwa kusimamia kambi za kifo ambapo mamilioni ya Wayahudi na wengine waliuawa.

Msemaji wa Adidas Oliver Brüggen alikanusha kukusudia kuunda jezi inayofanana na nembo za Nazi .

Chanzo: Bbc