Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Ujerumani wapanga kuivuruga Liverpool

Jurgen Klopp Changes.jpeg Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp

Tue, 12 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp ametajwa kuwa mrithi sahihi wa Hansi Flick baada ya kutimuliwa katika timu ya taifa ya Ujerumani.

Uamuzi huo umefuata Ujerumani kupokea kichapo cha mabao 4-1 ilichopata Ujerumani katika mechi ya kirafiki dhidi ya Japan, juzi.

Licha ya Klopp kuweka wazi kwamba atajitolea zaidi kuinoa Liverpool, lakini alikiri litakuwa jambo la kujivunia endapo atakifundisha kikosi cha Ujerumani ambako ndiko kwao.

“Kazi ya kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani ni jambo la kujivunia. Hakusa maswali kuhusu hilo, lakini siwezi kuondoka Liverpool kwa sasa halafu nikaifundishe kwa muda mfupi. Huwezi kufanya kazi kwa namna hiyo kama ikitokea natakiwa kuwepo muda wote kwa ajili ya timu,” alisema Klopp.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live